SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa mpira wa
miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa
utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Riziki
Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na
Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha
mtihani huo kinyume cha taratibu.
Naye
Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya
usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si
kweli.
Kwa
mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili
ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini
kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.
Wakati
huo huo: Stand United ya Shinyanga imekata rufani TFF ikipinga Kanembwa
JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo
kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi
hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari
16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo
Kanembwa JKT iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika
rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT
ilichezesha wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume
na maelekezo kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa
katika dirisha dogo hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji
wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu
Juma, Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji
Ismail, Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David
Sabugowiga.
Dirisha
dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo
Stand United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao
matatu kwa Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali
mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT
kugomea pigo la penalti dhidi yao.
CHANZO: KENGETE
0 comments :
Post a Comment