Mwanasheria
wa Idara ya Polisi ya Taifa ya Kenya Alexander Muteti ametoa wito wa
kufanya uchunguzi baada ya polisi kushindwa kumpata mtuhumiwa
aliyetoweka baada ya uvamizi katika Masjid Mussa mapema mwezi huu, The
Standard la Kenya limeripoti.
Hemed Salim Hemed alitoweka baada ya kukamatwa kwake katika msikiti na tangia hapo hajaonekana. Wiki iliyopita familia yake ilipeleka hoja katika Mahakama Kuu ya Mombasa ikitaka polisi wamtoe, ikidai kwamba polisi ama ilikuwa ikimshikilia katika mahali pasipo julikana au ilikuwa ikificha kifo chake.
Muteti, akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mwendesha mashataka, alidai kwamba Hemed alitoroka katika mikono ya polisi alipokuwa akipelekwa katika kituo cha polisi cha Makupa. Aliiomba mahakama kuagiza uchunguzi kufanywa na Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi ili kujua kilichotokea.
Mwanasheria wa familia Yusuf Abubakar alitoa wito wa kukamatwa kwa maofisa wa polisi waliokuwa wakimlinda mtuhumiwa na kushtakiwa kwa mauaji. Ombi lake liliungwa mkono na mwanaharakati wa haki za binadamu Okoiti Omtatah, ambaye alisema maofisa wa polisi wote walioshiriki katika uvamizi wanapaswa kukamatwa na kushtakiwa.
Muteti alisema ofisa yeyote ambaye uchunguzi utamtaja kuhusika na kutoweka kwa Hemed atashitakiwa ipasavyo.
Hemed Salim Hemed hajulikani alipo mpaka sasa |
About Unknown
0 comments :
Post a Comment