Halmashauri
aya Jiji la Arusha imevunja nyumba zake338 baada ya kushinda kesi
iliyofunguliwa na wapangaji Sangito Sumari na wenzake 216 katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha.
Operesheni
hiyo inayojulikana kama “Operesheni Mongela”ilianza saa 12 asubuhi jana
kwa kuvunja nyumba 56 eneo la Kilombero, nyumba 198 eneo la Kaloleni na
nyumba 84 katika eneo la Themi.
Wengi
walitegemea kuibuka vurugu wakati wa uvunjaji nyumba lakini hadi mchana
hapakuwa na pingamizi kwa wapangaji badala yake wenyewe walihamisha
vitu vyao mapema jana asubuhi kabla ya zoezi la kuvunja kuanza.
Hata
hivyo kuvunjwa kwa nyumba hizo kumeleta neema kwa baadhi ya watu
wakiwamo vijana wanaokusanya vyuma chakavu kuvamia maeneo hayo na
kuokota kila aina ya chuma au kitu ambacho waliamini kinaweza kuuzwa na
kuwapatia fedha.
Akiwa eneo la Kaloleni baada ya kukamiliza kuvunjwa nyumba za Kilombero,
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mongela alisema, ‘Operesheni Mongela’ ilipata
baraka zote za viongozi wa Serikali wanasiasa wakiwamo madiwani wote
Mbunge na Meya wa Jiji.CHANZO FATHER KIDEVU
CHANZO:MATUKIO NA VIJANA
0 comments :
Post a Comment