Picha kutoka maktaba
Kesi inayomkabili Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Nchini Tanzania, Sheikh Ponda lssa Ponda imeahirishwa tena Mpaka tarehe 21 Mwezi huu.
Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro Sheikh Issa Ponda anakabiliwa na mashitaka matatu imeahirishwa kutokana na jalada la kesi hiyo kuwa mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Mahakama imesema kwamba jalada la kesi hiyo lilihitajika mahakama kuu tangu mwezi oktoba na bado halijarudi. Kwa mujibu wa mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro imesema kesi hiyo itaendelea kutajwa mahakamani hapo mpaka jadala la kesi hiyo litakapoletwa.
Kesi hiyo iliyokuwa ianze kusikilizwa leo ambapo upande wa mashtaka ulikuwa umejiandaa kutoa ushahidi kuhusu kesi inayomkabili shekh ponda.
Mwezi agosti, Wakili wa Serikali, Benard Kongola alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate kuwa Sheikh Ponda alitenda makosa ya uchochezi Agosti 10, mwaka huu saa 11.45 jioni kwenye maeneo ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro.
Alisema siku hiyo, Sheikh Ponda alialikwa kutoa maelezo machache kwenye Kongamano la Eid lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri Mkoa wa Morogoro (Uwamo) na kwamba akiwa hapo alitamka maneno:
“Ndugu Waislamu, msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige sana,” huku akijua kutoa maneno hayo ni kosa kisheria.
Alisema kwa kufanya hivyo, Sheikh Ponda anayetetewa na mawakili watatu wanaoongozwa na Juma Nassoro, alivunja masharti ya Mahakama ya kifungo cha nje iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9, mwaka huu iliyokuwa imetamka kuhubiri amani.
Katika shtaka la pili, Sheikh Ponda anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai kwa kuwaambia:
"Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu, lakini haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo waliokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.”
Shtaka la tatu ni kudaiwa kutamka maneno yaliyoumiza imani ya watu wengine kama yalivyo katika shtaka la pili.
Baada ya kusoma mashtaka hayo, Kongola alisema walikuwa na mashahidi 15 na vielelezo vitatu ambavyo ni DVD mbili na kibali kilichotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro(OCD), Agosti Mosi, 2013 cha kongamano husika na hati ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, Mei 9, 2013.
Sheikh Ponda amerudishwa rumande.

About Omari Makoo
MIMI NNACHO SHANGAA KATIKA NCHI HII WANAOCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI WAKO WENGI SANA LAKINI AKISIMAMA SHEKH ANAEJITAMBUA NA KUWAFUNGUA MACHO WAUMINI WAKE KUHUSU HALIHALISI YA MAMBO YA NAVYOFANYIKA BASI ANATANGAZIWA UCHOCHEZI NAWATU WANAIMBISHWA NYIMBO ZA SHEKH HUYO KUWA MCHOCHEZI MPAKA WIMBOHUO UNASHIKA NAMBA 1 KTK TOP 10.TAFAKARI CHUKUA HATUA!!! DEMOUBAGUZI NASIO DEMOCRACY.
ReplyDelete