-->

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA ZITTO KABWE,MWIGULU NCHEMBA NA PETER MSIGWA BAADALA KUFANYA VIBAYA KWENYE UCHAGUZI WA MADIWANI

Zitto Kabwe

Kuondoa ukiritimba wa chama kimoja ili kujenga mfumo imara wa vyama vingi imekuwa ndoto yangu kwa miaka 20 sasa ( ending single party dominance). Matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Jana yanaumiza, yanavunja moyo na kuchukiza sana. Ni dhahiri kuna haja kubwa kukonga nyoyo za wananchi kwa sera na majawabu ya matatizo yao badala ya mitindo ( content over style).
Unapojali mitindo badala ya sera utaishia kutafuta sababu za kushindwa badala ya kuweka mikakati ya kushinda.
Nalaani kwa nguvu zote matukio ya fujo na umwagaji damu katika chaguzi zilizopita. Siasa za sera hazina fujo wala vurugu. Siasa za sera ndio siasa zinazojali wananchi. Twende huko....
 
 
 
Wana Chama na wapenzi wa chadema ,Iringa MJINI , niwapongeze kwa kazi nzuri na ngumu ya kufanya kampeni nduli, tumefanya kazi kubwa sana , kwa kiwango kikubwa tumejenga Chama na mtandao wetu umeongezeka. Hatupaswi kukataa tamaa , this is not the end of the word maisha yanaendelea,...wote kwa pamoja tunajua nguvu ya pesa ilivyotumika na BAADHI ya matajiri wenye masilahi BINAFSI na nduli.mimi najihesabia kuwa sisi ni washindi. Dhamira zao na nafsi zao zinawasuta kwa Yale maovu waliyoyafanya. Tuendele kujenga Chama chetu.
 
 


Kazi imekwisha Hongereni Watanzania hamjadanganyika na chopa zao wala sera zao Mbovu....Bado Mna Imani na Chama chenu CCM
Poleni watani Tukutane rasmi 2015 Huu ni mwanzo ... tuu ni rasha rasha tuu
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment