-->

TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU WA KAMATI KUU YA CHADEMA. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UTANGULIZI

Ndugu wanahabari, mbele yenu ni
muunganiko wa wawakilishi wa matawi
189 ya chama cha demokrasia na
maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja
huu wa matawi unawajumuisha
wajumbe kutoka majimbo yote ya
mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi
tarehe 30.nov 2013 kuanzia saa nne
asubuhi mpaka saa tisa kasorobo,
pamoja na mambo mengine
tumeazimia kuanzisha umoja huu wa
wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba
viongozi wetu wanaotuwakilisha
kwenye vikao vya maamuzi kama vile
wilaya, mkoa na
taifa wamekuwa waoga na
wameshindwa kuwakilisha mawazo
yetu tuliyowatuma badala yake wengi
wao wamekubali kuwa vibaraka wa
kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa
chama chetu na chama kingine
chochote kile cha siasa, uimara na
uhai wake unatokana na uwepo wa
misingi na matawi ya chama, hivyo sisi
wanachama wa matawi haya 189
tumeamua kuunganisha nguvu zetu
kutetea chama chetu na kuhakikisha
haki, heshima, katiba na maadili ya
chama vinafuatwa bila ya kuogopana
wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema
kuutaarifu umma wa watanzania na
wapenzi na wanachama wa chadema
mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema ni chama cha siasa
kinachopaswa kuendeshwa kwa
misingi ya kufuata taratibu, kanuni na
katiba yake na si vinginevyo. Lakini
badala yake kwasasa kumeibuka
ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa
juu kujitwalia mamlaka ya chama
kinyume na matakwa ya katiba ya
chama chetu hususan katika kutoa
haki sawa kwa viongozi na
wanachama wa chama chetu.
Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya
juu sana kwa wale wanao amini kuwa
ndani ya chama hawawaungi mkono
hivyo kupelekea kuwaadhibu kama
ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza
bila kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu
hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe
20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi
Mh: Zitto Zuberi Kabwe ,Dr. Kitila
Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba ,
kumeonyesha dhahiri si woga tu wa
Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki
wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu
kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio
cha kusaliti na uhaini ndani ya chama.
Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6
Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f)
Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji
ndani ya chama. Kulikuwa na haraka
gani ya kufanya maamuzi bila kufuata
taratibu hizi kwa viongozi hawa,
tuonavyo sisi baadhi ya wanachama
huo ni umangi meza na udhalilishaji wa
kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi
wetu waliotumia nguvu zao na akili
nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa
viongozi hawa ni
1. Kutaka kujua mapato na
matumizi ya fedha za chama
zinazotokana na Ruzuku ya
fedha za serikali.
2. Michango ya wanachama na
wapenzi kwenye mikutano ya
wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza,
Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka kujua taratibu za
manunuzi ya rasilimali ya
chama namna walivyopatikana
wadhabuni wa kusambaza
bendera na kadi za chama,
magari na pikipiki ambapo
ununuzi wake ni wa mashaka
makubwa.
5. Kutaka kuona usawa wa
kimadaraka kwa viongozi wote
bila ubaguzi wa aina yoyote
kuanzia ngazi ya chini mpaka
Taifa kinyume na ilivyo sasa
hasa makao makuu ya chama
ambapo ukanda na ubaguzi wa
hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
Mwenyekiti na katibu mkuu
wameshindwa kutatua migogoro ya
viongozi na wanachama kutoka
mikoani kwa njia sahihi za vikao na
kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa
viongozi na wanachama kutumia njia
ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na
katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza
mara kwa mara kwenye mitandao hiyo
hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya
mambo mbalimbali ya husuyo
maswala ya chama ilihali akijua
kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa
chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao
ilipelekea migogoro mikubwa sana
hususan mkoa wetu wa Mwanza na
kupelekea kupoteza Halmashauri ya
Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa
kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa
uongozi wa mkoa na wabunge kuwa
juu ya chama na kutumia nafasi zao
kuopanga safu za uongozi wanao
uwona watawatumikia wao na si
chama, hivyo kusababisha mifarakano
mikubwa ndani ya chama na kupelekea
kuvuliwa uongozi kwa viongozi
mbalimbali katika mkoa wetu kwa
maamuzi yasiyo zingatia utafiti na
uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa
vinara wa kuvunja katiba Mfano:
Kitendo cha kutoa muongozo nje
na matakwa ya katiba juu ya
kuwapata wawakilishi kwenye
vyombo vya maamuzi kama
wabunge kwamba wanaohitaji
kugombea 2015 waandike barua
makao makuu na wao ndio watatoa
wagombea kinyume na katiba ya
chama Ibara 7.2.13 inayotoa
taratibu ya kuwapata wagombea,
huwo ni uvunjaji wa katiba na
ubakaji wa demekrasia ndani ya
chama, sizani kama kuna uhaini
zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa,
Je, kama leo sisi Chadema
hatuheshimu katiba yetu
tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje
siku tukikabidhiwa nchi yenye watu
wenye mawazo na mtizamo tofauti
na sisi?. Hatutaki kuamini kama
nchi hii inaweza kugeuka uwanja
wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani
zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa
Arusha Mjini Mh: Godbless Lema
kumkashfu kiongozi wa chama Mh:
Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na
Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii
pia tunataka kujua hatua gani
zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw
Henry Kilewo kwa kuweka waraka
unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto
mbao chama makao makuu kupitia
kwa mkurugenzi wa habari na uenezi
wa chama kukana mbele ya vyombo
vya habari kuwa waraka huo chama
hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini
chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia
ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa
wa Kinondoni kichama, waraka huo
ambao chama kiliukana yeye aliweka
kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya
hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi
wa chama kuhusu maadili ya viongozi
kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani
zilizochukuliwa kwa waandaaji wa
tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya
siri kuhusu Zitto kwasababu tayari
makada na viongozi wetu wamelidhihiri
kuwa wao ndo miongoni mwa
waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu
wamelifumbia macho na kupelekea
kwetu baadhi ya wanachama kuamini
zengwe hili la kumchafua Zitto Lina
Baraka zote za viongozi wa chama
ngazi ya juu.
Tunataka kuona nguvu iliyotumika
kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa
kuandaa waraka ujulikanao kama
mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu
hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia
njia chafu ya kuandaa waraka wa
kumchafua zitto ambao chama
kinawajua na baadhi yao tumewaweka
humu kwenye tamko letu.
Kingine tunataka kwa mara nyingine
kwa viongozi wa chama makao makuu
kuwaambia umma wa watanzania ni
kwanini waraka huo huo uinaoitwa
warajka wa siri kuhusu Zitto leo
viongozi na wanachama mikoani na
kwenye majimbo waraka huo
uangawiwa kwa wanachama na
wananchi kwa agizo la makao makuu
kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha
viongozi wetu kuendeleza utawala wa
kibabe na kupelekea kuhatarisha
maisha ya baadhi ya wanachama na
viongozi wanaotofautiana nao
kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya
baadhi ya viongozi na makada wa
chama chetu wasiokuwa na uwezo wa
kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta
muda mwingi wa kutumia maneno ya
uchochezi dhidi ya wanachama na
viongozi wanaokinzana nao kifikra na
kimtizamo na kuhamasisha
wanachama wasiojua itikadi vizuri ya
chama kuwa wawashughulikie na
maneno haya yamekuwa yakisemwa
hadharani kwenye mikutano mbalimbali
hivyo wananchi wapenda Demokrasia
ya kweli kubaki na maswali magumu
kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali
kuhusiana na jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru
mara moja ili kupisha uchunguzi wa
mapato na matumizi ya fedha za
chama ambazo zinatokana na kodi za
wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na
katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya
kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele
cha ukomo wa uongozi ndani ya
chama kutangaza uchaguzi huku
mkiwaondoa washindani wenu ni
uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Mwisho tunataka maamuzi haya
HARAMU kamati kuu yabatilishwe na
mchakato wa kuwavua viongozi hawa
nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni
kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo
tarehe 4/12/2013 tutaungana na
wapigania Demokrasia kote nchini
kufanya maandamano yasiyokuwa na
ukomo mpaka uongozi uliopo utoke
madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo
muhakikishe mnawaamisha wabunge
vibaraka wote wa chadema mkoa wa
mwanza, wamchukue wenje
wakamtafutie jimbo moshi na highness
kiwia wamtafutie jimbo HAI na
MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa
sio saizi yao na tunataka waondoke
mara moja. Kinyume na hapo
tutawaondoa huku wakishuhudia kwa
macho yao.
Tunamuagiza mbowe na slaa
wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya
kanda ya ziwa ikiwa bado
hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi
yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa
wsatumwa wa fikra ndani ya chama
chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama
hiki vya kutosha, tumedharirishwa
kwenye chama hiki vya kutosha,
tumeburuzwa na kupuuza kwenye
chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya
mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,
tunasema kwamba kanda ya ziwa na
magharibi watupo chadema kwa bahati
mbaya, tupo humu kama wapokezi na
waasisi wakuu wa chama hiki,
tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina
Marehemu Bob Nyanga Makani,
Marehemu Balozi ngaiza Marehemu
Chacha Zakayo Wangwe, kamanda
Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe,
hatutaweza kukubali aina yoyote ya
upuuzi huu unaoeneawa na
kusimamiwa na WAHUJUMU
DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA
VEMA
ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya
CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA
CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya
ILEMELA
0757 084776
Source: Tamko la Umoja wa Matawi ya
WanaCHADEMA Mwanza juu ya
uamuzi wa Kamati Kuu - wavuti.com
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment