Polisi
wa kike wa kiislamu katika mji wa edmonton magharibi ya Canada, jimbo
la Alberta sasa wameruhusiwa kuvaa hijabu wakiwa ndani ya sare ya jeshi
hilo la polisi.
Kabla ya uamuzi wa kurekebisha vazi hilo washonaji wa hijab, kitengo cha polisi mbinu za mafunzo,timu ya haki za binadamu, walishirikiana kubuni hijabu hiyo inayofunika eneo lote la kichwa isipokuwa sura.
Taarifa iliyotolewa na Edmonton Police Services (EPS) inasema inaheshimu uchaguzi wa mwanamke wa kiislamu kuvaa hijabu.
"EPS inaendelea kubadilika mara kwa mara, kama kuwa na idadi zaidi ya polisi, haki na kushirikiana na taasisi za kipoli katika mataifa ya magharibi ambayo tayari yamekuwa na
sare kwa ajili ya vazi la hijabu",ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inatoa sababu kwa nini imeruhusu askari wa kike wa kiislamu kuvaa hijabu kwamba, "baada ya kupima kwa umakini, kwamba uvaaji hijabu hautaleta hatari yoyote,
au kupunguza ufanisi au kuathiri mwingiliano wa kijamii".
Akizungumzia taarifa hiyo Soraya zaki Hafez rais wa Edmonton wa baraza la wanawake wa kiislamu wa Canada, anasema, "Hii inafanya wanawake wa kiislamu kuwa sehemu ya jamii ya kipolisi".
Hafez alifurahi kuhusu idhini ya kubuni sare mpya kwa ajili ya maafisa wa polisi wa kike wa kiislamu. Kutokana na ruhusa hiyo Hafez anasema hatua hiyo inaweza kuwafanya wanawake wengi wa kiislamu kufikiria kufanya kazi polisi.
"Nadhani mikoa mingine itafuata nyayo", aliongeza.
.
Waislamu nchini Canada wanakadiriwa kuwa ni asilimia 2.8 katika taifa hilo lenye watu milioni thelathini na mbili na laki nane.

0 comments :
Post a Comment