-->

JE UNAFAHAMU SABABU YA MFASIRI WA LUGHA YA ALAMA KUKOSEA KWENYE IBADA YA HAYATI NELSON MANDELA??BOFYA HAPA KUFAHAMU

 
Thamsanqa Dyantyi mfasiri wa lugha za ishara anayelalamikiwa
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha Nelson Mandela imekuwa ikidanganya kwa miaka mingi na imekuwa ikitoa wafasiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mfasiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mfasiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kilikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment