Meja Jenerali Mohammad Ali Jafari Kamanda Mkuu wa Jeshi la
Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu Iran, Sepah amesema kuwa, nguvu za jeshi
hilo haziwezi kushindwa hata kama watashambuliwa kwa maelfu ya mabomu ya
adui. Meja Jenerali Jafari ameeleza kuwa, hata kama leo adui
atashambulia kwa maelfu ya mabomu, ni asilimia 10 hadi 20 tu ya nguvu za
Jeshi la Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu ndio zinazoweza kuharibiwa na
kwamba uwezo wa jeshi hilo hauishii tu kwenye makombora bali ni nguvu za
kistratejia. Matamshi hayo yametolewa kujibu madai kwamba Marekani
inaweza kuuzuia usifanye kazi mfumo mzima wa ulinzi wa Iran kwa bomu
moja.
Kamanda wa IRGC ameongeza kuwa, makombora ya Iran yanaweza kufika hadi Israel na kwamba wanaweza pia kuongeza uwezo wa makombora hayo lakini kwa sasa yana uwezo wa kufika hadi kilometa 2,000.
CHANZO:IRANI SWAHILI RADIO

0 comments :
Post a Comment