Maafisa katika eneo la kaskazini
mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa zaidi ya watu mia mmoja wameuwawa
katika shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu wa
Boko Haram.
Shambulizi hilo katika kijiji cha Izghe katika
jimbo la Borno linajiri siku nne pekee baada ya watu 39 kuuwawa katika
shambulizi jingine.Seneta wa jimbo la Borno Mohammed Ali Ndume ameiambia BBC kwamba watu mia moja na sita waliuwawa katika shambulizi hilo la hivi punde.
Amesema takriban wanamgambo mia moja walivamia mji wa Izghe jumamosi usiku. Wananchi waliokuwa wakikimbia mashambulizi hayo wamethibitisha kuwa takriban wanaume thelathini walikusanywa na kisha kupigwa risasi.
"Wamewauwa watu 106. 105 mia moja na tano ni wanaume na mwanamke mmoja kikonge aliyekuwa akijaribu kumlinda mjukuu wake wa kiume. Nadhani alipigwa risasi na kisha akafa."
Kisha wanamgambo hao walienda nyumba hadi nyumba wakiwauwa watu-wengi wao wakiwa ni wanaume. Baadhi walipigwa risasi huku wengine wakichinjwa.
Msemaji wa jeshi hakutoa maelezo kuhusu kisa hicho cha hivi punde lakini ameiambia BBC kwamba jeshi haliwezi kuwa kila mahali na kusema kuwa wanamgambo hao ni watu wa kuhamahama.
CHANZO:BBC SWAHILI
0 comments :
Post a Comment