
“Kuna
majangili 40 waliotambuliwa na tumetambua mtandao mzima, pale Arusha
kuna mtu mkubwa alikuwa anaendesha biashara. Kazi ilikuwa ni kutambua
mtandano wote, ule mtandao ni mpana sana,” alisema Rais Kikwete
Rais Kikwete alisema:
“Wakati
wa uhuru Tanzania ilikuwa na tembo 350,000… Mwaka 1987 walibaki
55,000…Juhudi za kupambana na ujangili zimeanza muda mrefu. Tangu mwaka
1989 kulikuwa na Operesheni Uhai na tulifanikiwa, kwani mwaka 2009 idadi
ya tembo ilifikia 110,000,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mwaka 2010
kulizuka aina nyingine ya ujangili na hii ni ya upuuzi kabisa. Kwa mfano
katika pori moja kulikuwa na tembo 30,000 na wote walikwisha… Ni jambo
gumu sana.”
“Nchi zilizoendelea kama Uingereza na Marekani watatusaidia katika
mafunzo na vifaa, silaha, uangalizi na vyovyote vile watakavyojitolea.”
0 comments :
Post a Comment