November
26 2013 ndio ilikua siku ya kumi toka shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kutangaza mgao wa siku kumi kwenye baadhi ya mikoa nchini
Tanzania ukiwemo 88.5 Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Felchesmi Mramba amezungumza
kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema ‘ni kweli kama
tulivyotangaza mgao wa Umeme kuchukua siku kumi kutokana na matengenezo
yale ya songosongo na kazi imeshakamilika na mgao umekwisha, nataka
kuwapa habari hizi njema za furaha watumiaji wa Umeme kwamba adha
waliyoipata imefikia mwisho’
millardayo.com : Vipi kama kuna watu bado wataendelea kulalamika kupata mgao wa Umeme?
Mramba : Kama mtu akiona kuna mgao naomba nitoe namba yangu, yeyote
atakaeona mgao anipigie 0767 042 009… bado tunatumia mitambo ileile ya
Songosongo pamoja na mitambo ya mafuta ya kwetu huku ndio tunatumia,
kidogo hali ya maji sio nzuri lakini maji kidogo yaliyopo yanachangia
kwa hiyo tukiunganisha nguvu zote hizo na mitambo ya dharura ya mafuta
ndio tunapata umeme wa kuwapa Watanzania’
Blogger Comment
Facebook Comment