Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri ushirika wa Segerea limenusurika kuteketea kwa
moto baada ya watu wasiojulikana kutupa chupa iliyodhaniwa kuwa na
mafuta ya taa au ya petroli na kulipuka ndani ya kanisa na kuunguza
baadhi ya vitu vilivyowemo katika madhabahu ya kanisa pamoja na gari
lililokuwa nje ya kanisa hilo majira ya saa 8 usiku usiku wa kuamkia
leo.
Itv
imefika katika kanisa hilo na kukuta baadhi ya vitu vilivyokuwa
madhabauni vikiwa vimeungua vibaya kikiwemo kitabu kitakatifu cha
biblia, huku kukiwa na michanga mingi sakafuni baadhi ya vyombo vya
muziki vikiwa vimeparaganyika wakati waumini wa kanisa hilo walipokuwa
katika jitihada za kukabiliana na moto huo usilete madhara.
Akielezea
tukio hilo mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Segerea Bwana Noha
Kipingu, amesema limetokea majira ya saa 8 za usiku wa kuamkia leo
,wakati baadhi ya waumini wakiwa ndani ya kanisa katika maombezi ya
yaliyoanza saa 4 usiku kwa ajili ya mkutano unaotarajiwa kufanyika
jumapili ya agosti 25 mwaka huu.
Akielezea
msimamo wa kanisa KKKT usharika wa Segerea kuhusu tukio hilo, licha ya
kusisitiza linachukuliwa kama sehemu ya matukio mengine ya ulipuaji wa
makanisa yanayoendelea,amesema kwa mujibu wa maelezo ya mlinzi wa kanisa
ameona watu wanne waliotega chupa na kulipua kwenye gari la kanisa
pamoja na kurusha chupa nyingine ndani na kisha kukimbia.
Baadhi
ya waumini walionusurika katika tukio hilo wamesema wamesikia mshindo
mkubwa wa kitu kinachofanana na bomu katika madhabau ya kanisa hilo
wakati wakiwa wamesimama mbele ua kanisa hilo na kisha moto ukaanza
kuunguza madhabau hali iliyowafanya kukimbia na kisha kurudi ndani kwa
ajili ya kuzima moto huo.HABARI NA ITV
0 comments :
Post a Comment