Polisi Makao Makuu Kitengo cha Makosa ya Jinai Rasimali Watu, juzi
ilimhoji Amir Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa
Kundecha kwa kile walichodai kuwa mtu huyo ni rafiki mkubwa wa Sheikh
Kondo Bungo anayetafutwa polisi.
Taarifa kutoka kwenye vyanzo
vya polisi Makao Makuu zilieleza kuwa Bungo anatafutwa na polisi kwa
kile walichodai alitoa maneno ya uchochezi katika Mkutano wa Waislamu
uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Kamishna Msaidizi wa
Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi, kutoka Kitengo cha Upelelezi Makao
Makuu alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, simu yake ilikuwa
haipatikani.
Chanzo chetu kilidokezwa kuwa baada ya mkutano huo
ambao pia ulihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert
Kiondo, Polisi walipanga kumkamata Bungo kwa wakati maalumu na siyo eneo
lile ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea endapo angetiwa
nguvuni.
“Kundecha aliitwa jana (juzi) na kuhojiwa kwa saa
kadhaa na kumtaka amlete Bungo ambaye ni mtu wake wa karibu, “ alisema
mtoa habari huyo kuongeza kuwa: “Asipofanya hivyo kwa muda aliopangiwa
basi atakamatwa yeye hadi hapo atakapo patikana Bungo.”
CHANZO: Mwananchi
Polisi Makao Makuu Kitengo cha Makosa ya Jinai Rasimali Watu, juzi ilimhoji Amir Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha kwa kile walichodai kuwa mtu huyo ni rafiki mkubwa wa Sheikh Kondo Bungo anayetafutwa polisi.
Taarifa kutoka kwenye vyanzo vya polisi Makao Makuu zilieleza kuwa Bungo anatafutwa na polisi kwa kile walichodai alitoa maneno ya uchochezi katika Mkutano wa Waislamu uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi, kutoka Kitengo cha Upelelezi Makao Makuu alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, simu yake ilikuwa haipatikani.
Chanzo chetu kilidokezwa kuwa baada ya mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, Polisi walipanga kumkamata Bungo kwa wakati maalumu na siyo eneo lile ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea endapo angetiwa nguvuni.
“Kundecha aliitwa jana (juzi) na kuhojiwa kwa saa kadhaa na kumtaka amlete Bungo ambaye ni mtu wake wa karibu, “ alisema mtoa habari huyo kuongeza kuwa: “Asipofanya hivyo kwa muda aliopangiwa basi atakamatwa yeye hadi hapo atakapo patikana Bungo.”
CHANZO: Mwananchi
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment