WAKATI leo kikiwa ni chungu cha tisa cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan, kumeibuka maajabu, mtoto wa kike amezaliwa akiwa amevaa
Tasbihi shingoni.
Tukio hilo lilijiri katika hospitali binafsi ya
uzazi kwenye Jiji la Kotaworo, eneo la Bida, jimboni Niger State nchini
Nigeria, Jumapili iliyopita ambapo maelfu ya watu walikusanyika kwa
lengo kumshuhudia mtoto huyo.
|
Mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa Tasbihi shingoni.
|
Kwa mujibu wa Mtandao wa Naija, mama wa
mtoto huyo, Adijat alikimbizwa hospitali karibu na nyumbani kwa Alhaji
Mohammed Bello Masaba, majira ya saa 8:00 mchana na baada ya pilika za
uzazi, alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Mmiliki wa hospitali hiyo
ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi
hilo la kujifungua alisema: “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na
Tasbihi nyeusi shingoni.
“Nilishangaa baada ya muda Tasbihi hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe.”
Mara
baada ya habari hiyo kusambaa, maelfu ya watu walifika hospitalini hapo
wakisema: “Allahu Akibar…Allahu Akibar (Mungu mkubwa…Mungu mkubwa).
Baada
ya taarifa hiyo ya ajabu kusambaa watu kutoka maeneo mbalimbali ya
nchini Nigeria walifurika kumwona mtoto huyo wengine wakimgusa.
Juhudi za kumpata baba wa mtoto huyo aitwaye Isah zilishindikana.
0 comments :
Post a Comment