Mohammed Morsi akiwa mahakamani
Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi
atafika katika mahakama moja mjini Cairo ili kusikiza mashtaka ya
upelelezi na njama ya kutaka kutenda ugaidi yanayomkabili.Bwana Morsi aling'atuliwa mamlakani na jeshi mnamo mwezi Julai na sasa anakabiliwa na mashtaka mengine matatu.
katika kesi hiyo yeye na wanachama wengine 35 wa vunguvu la Muslim Brotherhood wanatuhumiwa kwa kushirikiana na makundi ya kigeni kama vile Hamas,Walinzi wa mapinduzi nchini Iran na Hezbollah kupanga mashambulizi nchini Misri.
Iwapo atapatikana na hatia bwana Morsi anakabiliwa na hukumu ya kifo.
0 comments :
Post a Comment