WAKATI
keshokutwa Bunge Maalum la Katiba linaanza kukutana mjini Dodoma, Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema huenda kikasusia Bunge
Maalum la Katiba iwapo litaendeshwa kwa kufuata matakwa ya chama cha
siasa na siyo ya wananchi.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema hayo jana wakati akielezea
maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichofanyika jana na kueleza kuwa
chama hicho kinaenda katika Bunge hilo kikiwa na hadhari ya hilo.
Alisema
wanaenda kwenye kikao hicho wakiwa na masikitiko kutokana na uteuzi wa
wajumbe 201 wa bunge hilo waliotangazwa hivi karibuni kuwa karibu
asilimia 75 hadi 80 ni wanaCCM.
Akijibu
hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema “Tumewazoea, sio
mara ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni
Katiba isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”.
Naye
Mbowe alifafanua “Hatuendi katika bunge hilo kugoma lakini mambo
yakienda visivyo kwa kufuata matakwa ya chama cha siasa na siyo
mapendekezo ya rasimu ya pili ya Katiba hiyo ambayo ni ya wananchi
tutalizira Bunge hilo,” alisema.
Alibainisha
kuwa chama hicho hawatasita kurejea kwa wananchi wakati Bunge
likiendelea au likiwa limeisha iwapo wingi wa wabunge wa chama tawala
utaathiri Bunge hilo.
“Sasa
wananchi watatuelewa dhamira yetu ya kutaka wajumbe hao wasiteuliwe na
Rais kwani tulibishana sana lakini baadaye tulikubaliana jambo ambalo
limeonesha kwa kuteuliwa makada wengi kwa manufaa ya chama tawala,”
alisema Mbowe.
Alisema
ingefaa makundi yenyewe yangeteua wawakilishi wao na siyo kupeleka kwa
Rais hivyo Bunge hilo linaloanza keshokutwa wanaenda kwa tahadhari.
Vikao
vya Bunge Maalum la Katiba linatarajia kuanza keshokutwa likihusisha
wajumbe ambao ni wabunge wote wa Baraza la Wawakilishi ,Wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano na wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete akishirikiana na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein.
Wajumbe
hao 201 wameteuliwa kutoka makundi tofauti yakiwemo ya Taasisi zisizo
za kiserikali, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Taasisi za
dini, Taasisi za elimu, watu wenye ulemavu, vyama vya wafanyakazi, vyama
vinavyowakilisha wakulima, wafugaji, wavuvi na kundi la watu wenye
malengo yanayofanana.
Bunge
hilo litahusisha wajumbe takriban 650 wanaokwenda kuijadili rasimu ya
pili ya Katiba na watatumia siku 70 na iwapo hazitatosha wataongezewa
siku 20 ili kukamilisha mjadala huo. Kitakachofuata baada ya Bunge
Maalum la Katiba ni wananchi kupiga kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo
mpya.
Katiba
hiyo mpya itafuta Katiba ya sasa iliyodumu tangu Tanganyika ilipopata
uhuru mwaka 1961 na mabadiliko kadhaa yaliyofuatia baada ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
Alipoulizwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema “tumewazoea, sio mara
ya kwanza kususa waache wasuse najua nia yao tangu mwanzo ni Katiba
isipatikane. Katiba mpya itapatikana hata wakisusa”.
CHANZO:GUMZO LA JIJI
0 comments :
Post a Comment