Baadhi ya wanajeshi wa kulinda amani
Wanajeshi
wa kulinda amani wa Kimataifa walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati
wameingia nyumba hadi nyumba Bangui, kuwanyang'anya silaha wanamgambo
wanaoshutumiwa kutekeleza visa vya uhalifu dhidi ya Waislamu
waliowachache.
Oparesheni
hiyo ya kipekee ilifanywa na wanajeshi wa kulinda amani takriban 250
pamoja na polisi katika eneo jirani la Boy Rabe mjini Bangui, eneo
linalokaliwa na wanamgambo wa Kikristo.
Mashambulizi kutoka kwa Wanamgambo hao yamesababisha Waislamu kuukimbia mji huo katika wiki za hivi karibuni.
Kulingana
na Mwanasheria mkuu wa serikali Ghislain Gresenguet, mabomu pamoja na
silaha nyingine zilipatikana huku watu kadhaa wakitiwa nguvuni.
Kwa
upande wake mmoja wa wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika kikosi cha
MISCA aliliambia shirika la habari la AFP watu wote waliopatikana na
silaha wametambuliwa na watafikishwa polisi.
Wanamgambo
wa "anti-balaka" walijikusanya katika nchi hiyo ilio na idadi kubwa ya
wakristo kujibu mashambulizi ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na waasi wa
kiislamu wa Seleka baada ya kuuangusha utawala wa rais Francois Bozize
katika mapinduzi ya Machi mwaka 2013.
Katika miezi
ya hivi karibuni, kundi la wanajeshi wa Kimataifa waliopelekwa katika
taifa hilo ambalo ni koloni la zamani la Ufaransa, wamefanikiwa
kusimamisha mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na waasi wa Seleka na
wanamgambo wa Kikristo hali iliosababisha hofu miongoni mwa Waislamu.
Catherine Samba Panza, atangaza vita dhidi ya kundi la anti balaka.
Rais wa
mpito katika Jamhuri hiyo ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza,
ambaye ni Mkristo, wiki iliopita alitangaza vita dhidi ya kundi la anti
balaka. Mashambulizi ya kundi hilo yamesababisha kutolewa onyo la
kutokea ghasia za kidini.
Huku hayo
yakiarifiwa Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema
operesheni ya jeshi la nchi hiyo katika Jamhuri ya Afrika ya kati
zitakuwepo kwa muda mrefu kuliko ilivyopangwa hapo awali. Siku ya Ijumaa
Ufaransa ilisema itatuma wanajeshi wake wengine 400 katika Jamhuri ya
Afrika ya Kati.
Takriban
watu milioni moja wamepoteza makaazi yao kutokana na mapigano kati ya
makundi ya waasi wa Kiislamu wa Seleka na wanamgambo wa Kikristo. Watu
takriban 2000 wameuwawa katika ghasia hizo za kidini tangu mwezi wa
Desemba mwaka uliopita.
Ufaransa
na Umoja wa Ulaya umeahidi kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika nchi
hiyo ya Kiafrika wakati kukiwa na visa vya kuogofya katika ghasia za
nchi hiyo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana alisema Berlin
ilihitaji kupiga jeki ushirikiano wake wa kijeshi na Ufaransa hasaa
barani Afrika.
"Mahusiano
yetu ya karibu yanawezekana", Alisena Kansela wa Ujerumani huku
akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni wa kuungana pamoja katika mataifa ya
Mali, ama Jamhuri ya Afrika ya kati.
Chanzo, dw.dw/swahil
0 comments :
Post a Comment