Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara,
kimeomba radhi kwa chama cha waandishi wa habari mkoani humo (MRPC)
kutokana na kitendo kilichofanywa na wafuasi wa chama hicho tawala, kwa
kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi na kusema kuwa
waliohusika watachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara,
Christopher Sanya, alisema wanaomba radhi kwa mwandishi huyo,
Christopher Maregesi pamoja na kwa waandishi wote wa habari wa Mkoa wa
Mara
“Mimi kwa niaba ya chama ninaomba radhi
kwa kitendo alichofanyiwa….ninakikemea kwani si cha kiungwana,”alisema
Sanya na kuongeza: “Tutafanya uchunguzi na wale watakaobainika kuhusika
tutawachukulia hatua.”
Aliongeza: “CCM tunathamini mchango wa waandishi wote kwa ujumla, hivyo kitendo kilichofanywa si cha kiungwana.”
Maregesi alishambuliwa Februari 8 mwaka
huu na wafuasi wa CCM mjini Bunda, muda mfupi baada ya kumalizika kwa
mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho katika
Kata ya Nyasura.
CHANZO:MALUNDE
0 comments :
Post a Comment