-->

CHADEMA WATOA UFAFANUZI WA MATUMIZI YA CHOPA KWENYE UCHAGUZI WA MADIWANI



Kuna mambo mengi
yamezungumzwa tangu jana na
hadi leo kuhusu matokeo ya
uchaguzi wa marudio katika kata 27
na ushindi wa CHADEMA katika
kata 3 za Kiborloni, Sombetini na
Njombe mjini.
Tutaendelea kusoma, kusikiliza na
kupokea kila aina ya criticism,
zinazotolewa kwa njia mbalimbali,
ingawa hatimaye tutafanyia kazi
constructive criticism zinazojengwa
katika dhamira ya kweli na nia
njema kwa ajili ya mustakabali wa
Watanzania na chama chao,
CHADEMA.
Moja ya masuala yanayozungumzwa
na wapinzani wa CHADEMA,
ambayo hata leo katika press
conference iliyoitishwa Lumumba,
litazungumza sana, ni kujaribu
'kuoanisha' M4C-OPD (matumizi ya
chopa 3) na ushindi wa kata 3.
Kuoanisha mambo hayo kwa
mgongo wa kufanya uchambuzi au
tathmini ya mambo hayo mawili, ni
ama kuamua kuwa myopic kwenye
hoja muhimu au kuamua
kupotosha kwa makusudi ya
propaganda nyepesi au kutokujua
tu.
Wakati Mwenyekiti Mbowe
anazindua M4C- Operesehni
Pamoja Daima, mbele ya waandishi
wa habari alisema malengo ya
shughuli hiyo maalum kuwa
itaweka msisitizo au mkazo kwenye
masuala makuu yafuatayo;
Mchakato wa katiba mpya
Daftari la wapiga kura
Wazawa na rasilimali za nchi
yao
Ugumu wa maisha
unaosababishwa na uongozi
mbovu na sera zilizoshindwa
za CCM
Kwa wale waliofuatilia OPD, kila
mtu anajua namna ambavyo
imeibua mjadala mkali katika
masuala hayo, kuanzia na katiba
mpya, wazawa na matumizi
(unufaikaji) ya rasilimali, ugumu...
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
ikalazimika kutangaza kwamba
tayari serikali imetoa fedha za
kuboresha daftari la wapiga kura.
Haitoshi tu kusema hivyo. Viongozi
wakuu, Mwenyekiti Mbowe na
Katibu Mkuu Dkt. Slaa wakatoa
kauli ya chama wakiitaka NEC itoe
taarifa kamili juu ya mambo
kadhaa, ikiwa ni pamoja na;
Ratiba kamili ya shughuli hiyo
Lini NEC itaanza kukagua vituo
Tarehe rasmi ya kuanza
kuboreshwa daftari
Serikali imetoa bajeti ya kiasi
gani (inatosha kwa shughuli
nyeti kama hiyo?
Kwa sababu M4C-OPD ilikuwa ni ya
nchi nzima, yako maeneo ya
uchaguzi ambako chopa zilifika.
Lakini kuoanisha matumizi ya
chopper 3 na matokeo ya ushindi
wa kata 3, ni kulazimisha hoja
isiyokuwepo kwa premises za
kuokoteza Wapinzani wa CHADEMA
wakisukumwa na euphoria ya
ushindi usiokuwa na uhalali
(tutafafanua), wamejikita kwenye
'negative (ya picha)'
inayozungumzia chopper 3 kwa
kata 3, wanashindwa kuiona 'picha
kubwa' (negative Vs bigger picture),
inayozungumzia masuala kadhaa,
mfano;
Katika uchaguzi wa 2010 matokeo
yalikuwaje?
Je kuna mabadiliko ya goal post,
figures na namba?
Je mabadiliko hayo yako in favour of
status quo au yanasapoti vuguvugu
la mabadiliko?
CHADEMA itajikita katika hayo kwa
sababu ni muhimu sana katika
suala kulinda demokrasia ya watu
na kusheherekea ushindi, hasa
ushindi ulio halali.
Mfano; katika Kata ya Njombe
mjini, mwaka 2010 CHADEMA
haikusimamisha mgombea kabisa
wa udiwani wala ubunge. Mgombea
Urais wa CHADEMA alimzidi kwa
mbali mno mgombea urais wa
CCM. Mbali mno.
Matokeo ya jana katika kata hiyo
hiyo kwa uchaguzi wa udiwani,
yanaonesha kwamba;
CHADEMA imepata kura 2,202
CCM imepata kura 1,094
Jumla ya kura zilikuwa 3334
Jumla ya vituo vilikuwa 41, CCM
imeshinda kituo kimoja tu kwa
tofauti ya kura 9
Iko mifano mingi ya namna hii
katika uchaguzi wa jana. Kuna
maeneo ambayo CHADEMA
haikuwahi kuweka mgombea,
imetoa ushindani mkali na kuna
maeneo ambayo uchaguzi uliopita
kulikuwa na tofauti kubwa mno ya
kura, lakini safari hii gap
limepunguzwa kwa namba kubwa
sana.
Mfano Kata ya Mpwayungu, Mtera,
Dodoma Mwaka 2010
CHADEMA 602
CCM 1812
Mwaka 2014 (jana)
CHADEMA 555
CCM 872
Katika Kata ya Ubagwe, mwaka
2010, CCM ilipita bila kupingwa.
Uchaguzi wa jana umekuwa;
CCM 329
CHADEMA 215
TADEA 71
Zilizoharibika 3
Where are the voters? Where is
legitimacy?
Moja ya masuala ya msingi sana
ambayo tulitarajia yawaumize
kichwa sana watu, hususan walioko
madarakani ni swali hili; Je wapiga
kura wako wapi?
Suala hili limepewa uzito na
CHADEMA pamoja na wapenda
demokrasia na maendeleo wengine
wengi tu nchini tangu baada tu ya
matokeo ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2010. Nani anajali?
Walioko madarakani wangelikuwa
wanathamini mchakato wa
demokrasia ya uwakilishi, ambayo
maana yake ni kuwaheshimu watu/
wapiga kura, kamwe wasingekuwa
wanakimbilia kushangilia matokeo,
tena yasiyowapatia uhalali.
Mathalani
Kata ya Ubagwe, Ushetu, Shinyanga
Wapiga kura walioandikishwa wako
4270
Waliopiga kura jana ni 618
CCM wameshinda kwa kura 329
dhidi ya CHADEMA kura 215,
TADEA- 7, zilizoharibika 3.
Kata ya Nyasura Bunda,
Waliojiandikisha ni 5333
Waliopiga kura 1579
Wapiga kura wako wapi? Uko
wapi uhalali wa ushindi wa kata
nyingi? Aidha, wapinzani wa
CHADEMA hawataki kabisa kabisa
kuzungumzia irregularities. Very
serious irregularities done
purposefully. Hawataki kabisa
kugusia namna ambavyo watu
wamepigwa wazi wazi na
kuchukuliwa kwenye vituo vya kura,
wakiwemo mawakala wa CHADEMA
kisha eti wakapelekwa vituo vya
polisi.
Wapenda demokrasia hao ya
ushindi, hawataki kabisa
kuzungumzia mapanga na mashoka
yaliyotembezwa jana na Green
Guards!
Huwezi kuzungumzia kushindwa au
kushinda kwenye matokeo ya jana
au mengine yoyote yale, bila
kujadili masuala hayo kwa upana
sana, unless kama tumekubaliana
kuwa iwe ni sehemu ya demokrasia
yetu, watu kukatwa mapanga,
mashoka, damu kumwagika, watu
kukamatwa vituoni bila makosa,
kisha CCM wakaachwa wanafanya
wanavyotaka, wakuu wa wilaya
kuingia vituoni na kutoa maagizo.
Labda kwao ni sehemu ya mchakato
wa kuchagua wawakilishi!
Vinginevyo basi tuanze kuwaandaa
Watanzania kwa uchafu wa namna
hii.
Kwa kusema haya kamwe
haimaanishi kuwa CHADEMA
haihitaji kufanya tathmini ya
kitaalamu, kitaaluma na kina sana.
Itafanyika na itakuwa muhimu kwa
ajili ya kuendelea kujiimarisha na
kujipanga katika mapambano
haya.
Lakini kwa vyovyote ni muhimu
sana sana, kuweka mikakati ya
kukabiliana
na Intarahamwe inayotaka
kupandikizwa Tanzania na
Watawala dhidi ya Watanzania.
Suala hili la Green Guards kufanya
maovu dhidi ya wapinzani wa CCM
kwenye uchaguzi, tena mahali
pengine uovu wa kutisha
unaohusisha silaha, kwa namna ile
ile ya Intarahamwe, mbele ya askari
polisi, wala wasiguswe, wapo
wengine bado wanaliona kuwa ni
jambo dogo au mzaha fulani hivi.
Siku madhara yake yatakapokuwa
yameshafika mfupani,
tutajuaIntarahamwe ilikuwa ni kitu
gani, kilianzaje, kilipataje nguvu na
matokeo yake yalikuwa ni nini.
Where are the voters, where is
legitimacy?
Tumaini Makene
Afisa Habari-Chadema 

CHANZO:MAARIFA YA JAMII
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment