Klabu ya Etoile
Du Sahel imetoa taarifa rasmi kuhusu sakata lake na mshambuliaji wa
kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi anayekipiga katika klabu ya Yanga.
Mtandao huu
umefanikiwa kupata barua rasmi ya Etoile kwenda FIFA wakimshtaki rasmi
Okwi kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na hivyo kutaka walipwe fidia.
Katika barua hiyo Etoile wanaeleza: "Mwanzoni
kabisa alipoanza kuitumikia klabu, hatukuona tabia yoyote isiyoridhisha
kutoka kwake, alishiriki kwenye baadhi ya mechi rasmi za mashindano na
timu ya wakubwa na nyingine kadhaa kikosi cha U23, alilipwa mishahara
yake pamoja na bonasi kulingana na makubaliano ya mkataba, sheria na
kanuni za FIFA na shirikisho la soka la Tunisia.
"Baadae
tukagundua mabadiliko kwenye tabia yake, ilikuwa mwanzoni mwa mwezi May
2013, tulianza kuona utoro mazoezini bila sababu za msingi na mchango
wake kwenye timu ukaanza kushuka kwa kiasi kikubwa pamoja na kuwa mmoja
wa wachezaji tegemeo waliokuwa wamefuzu vigezo vyote kushiriki katika
mechi zinazoandaliwa na CAF.
"Sababu
pekee aliyokuwa akisema inamfanya agome kuitumikia klabu vizuri ni
madai ya bonasi pamoja na kwamba hakuwa amecheza mechi ambazo alikuwa
anadai hizo bonasi. Kwa mujibu wa sheria na kanuni za shirikisho la soka
la Tunisia ni kwamba bonasi na zawadi nyingine hutolewa kulingana na
namba ya mechi ambazo mchezaji amecheza na mechi za mashindano
alizoshiriki.
"Muda
mfupi baadae tulipokea mualiko wake kutoka Shirikisho la soka la Uganda
kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano ya kufuzu kombe la dunia 2014
dhidi ya Liberia na Angola, michezo iliyopangwa kufanyika tarehe 8 na 15
June 2013. Lakini Okwi aliondoka klabuni bila ruhusa kutoka kwa klabu
au kiongozi yoyote.
"Tulifanya
mawasiliano na shirikisho la soka la Tunisia, Uganda na mchezaji
mwenyewe ili aweze kurudi klabuni lakini akakataa muda wote.
"Tarehe
12, July 2013, tuliwasiliana FUFA katika kusisitiza mchezaji arejee kwa
sababu bado alikuwa na mkataba na klabu. Tunaamini mchezaji alikuwa
akidanganywa na baadhi ya watu ili avunje mkataba na klabu katika bila
kufuata sheria. Kitendo cha kuchelewa kwa mshahara hakimpi mamlaka ya
kuvunja mkataba kisheria.
"Ukosefu huu wa nidhamu wa mchezaji ulitufanya tuanze mchakato wa kudai fidia na hivyo tunawaandikia FIFA kuomba msaada wao.
*Ukosefu
wa nidhamu na kutojua majukumu yake kwa mchezaji kumesababisha hasara
kubwa za kifedha kwa klabu na hili limetufanya kuomba usaidizi kutoka
FIFA kuhusu yafuatayo:
-Kutokana na kwamba Emmanuel Anorld Okwi amevunja mkataba yeye mwenyewe na klabu yetu bila kuwa na sababu inayotosha kumpa haki ya kuvunja mkataba kisheria.
-Tunawaomba FIFA wampe mchezaji amri ya kulipa fidia kutokana hasara na aibu ya kimichezo aliyoingizia klabu:
i.
Two hundreds fifty seven thousands-one forty t two US.Dollars(247,142
USD) kama fidia ya as a compensation of prorata of the value of his
transfer (cf pj n.6)
ii. Ten thousands US dollars ( 10,000US D) for the period of May 2013 to June 2013( salaries and prizes)
iii. One hundred eighty thousands US Dollars (180,000 US D) for the
period of July 2013 to June 2016 ( salaries till the end of his
contract).
iv.Four hundreds eighty thousands US Dollars( 480,000) for the period of July 2013 to June 2016( prizes of the year 2015)
v.Charges for location of five hundreds US Dollars per months( 38months x500 US D= 19.000US D)
Costs for air plane tickets of one thousands US Dollars par months ( (1000US D x12= 12,000USD)
vi. Costs for hiring car of seven undred US D per month ( 700 US D x38= 26,000 USD)
vii. Salaries and prizes /bonuses already received by the player of fifty thousands US dollars( 50,000USD)
viii. Financial and sportive prejudice( for rupture/breaking legal the
contract during the protectedperiod and indemnity of his formation at
Etoile Sportive du Sahel) estimated value is three hhundreds thousands
US dollars ( 300,000 US D)
This
make the total amount to be paid by the player = One million three
hundred twelve thuousands seven hundreds forty two US Dollars( 1,312,742
US D)."
Hivi ndivyo
inavyosomeka sehemu ya barua ya Etoile kwenda FIFA kuhusiana na madai
yao dhidi ya Okwi. Watunisia hao ambao bado wanadaiwa na Simba kiasi cha
dola laki tatu, wameomba walipwe fidia ya dola millioni 1.3 ambayo
inaweza kuwa na thamani ya billioni na nusu za kitanzania
0 comments :
Post a Comment