-->

SERIKALI YA UGANDA YATANGAZA SIKU MOJA YA MAOMBOLEZO BAADA YA WATU ZAIDI YA 50 KUFA KWA MAFURIKO

Zaidi ya watu 50 wamefariki nchini Burundi baada ya kusombwa na maji pamoja na maporomoko ya udongo.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.
Majumba yamebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa
Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na kusombwa na maji.
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya maombolezi ya kitaifa hapo kesho.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment