Mtaalamu
wa kuteketeza meno ya tembo akipokea meno hayo kuyaweka kwenye mtambo
wa kuyateketeza. Ubelgiji leo imeteketeza tani 1.5 za meno ya tembo
yaliyokamatwa yakiingingizwa nchini humo.
Meno
ya tembo na Mtambo wa kuteketeza meno hayo. Leo hii Serikali ya
Ubelgiji imeteketeza meno ya tembo tani 1.5 iliyoyakamata yakiingingizwa
Ubelgiji. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala
ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi
nyingine zenye soko la meno hayo kuchukua hatua kama ilivyofanya
Serikali ya Ubelgiji. Aidha, Balozi Kamala ameziomba nchi zilizoendelea
kusaidiana na nchi zinazoendelea kupambana na ujangiri.
Naibu
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Mhe. Onkelinx akihutubia Wadau wa kupambana na
biashara ya meno ya tembo na kuzindua uteketezaji wa tani 1.5 za meno ya
tembo. Meno hayo yamekamatwa Ubelgiji katika jitihada za Ubelgiji
kupambana na biashara ya meno ya tembo. Balozi wa Tanzania Ubelgiji na
Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameipongeza Serikali ya
Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi za Ulaya kushirikiana na nchi
zenye mbuga za wanyama kupambana na ujangiri na kulinda tembo na
wanyama wengine.
0 comments :
Post a Comment