Nchini
Kenya kuna Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Naivasha ambae katengeneza
‘Ndege’ yake ambayo toka ameanza kuiunda alisema lazima ipae huku akiwa
katumia ( vifaa mbalimbali kutoka kwenye Bajaji kuiunda.
Kazi ilipokamilika nyumbani kwao
alipoitengenezea, Polisi wa mji huo wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni
kinyume na sheria lakini ili kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni
vyema akapata kibali kutoka kwa mamlaka ya anga.Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii ndege kutoka uwanja wa mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.
Hata
hivyo Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha Meru ana imani ataipaisha ndege
yake siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo hata hivyo ilipata
hitilafu kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali mbaya ya
uwanja huu iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule
ya upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya
kuhusu kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu.(awadh ibrahim)
0 comments :
Post a Comment