JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION
Mamlaka
ya Mawasiliano imebaini kuwa kuna mtandao wa matapeli wanaotumia jina la
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti inayojiita
“TCRA Foundation” na inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.
Tovuti inayotumika ni http://tcra-foundation.wix.com/tcrafoundation.
Mtandao
huu umetengenezwa wa kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali
zikiwaonyesha Raisi Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makawe Mbarawa na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.
Aidha
mtandao huu unadai kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Kampuni za Simu za
Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB na NMB zinashirikiana kuendesha
Foundation hiyo.
Mamlaka
ya Mawasiliano inawatahadharisha wananchi kuwa haina “Foundation” yoyote
ya kutoa misaada ya fedha. Mtandao huu unatumika kuwalaghai wananchi na
kuwaibia fedha zao kwa kuwataka watume fedha za kujiunga na mtandaqo
huo kwa number za simu za Tigo na Vodacom zinazoonesha kusajiliwa kwa
jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na
ni wizi na udanganyifu.
Mamlaka
ya Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na tahadhari na watu hawa ambao
hutumia mitandao ya Mawasiliano ya simu na intaneti kufanya utapeli.
Usitume fedha wala kujiunga na mitandao ya namna hii.
Aidha
Mamlaka ya Mawasiliano inawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa
taarifa wanapobaini utapeli wa namna hii kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka
kwa vyombo vingine vya usalama ikiwa watahisi au kuwa na taarifa za watu
wanaojihusisha na udanganyifu huu katika mitandao ya Mawasiliano ili
kuzuia vitendo hivi vilivyoshamiri katika siku za hivi karibuni.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
8Aprili 2014
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
8Aprili 2014
0 comments :
Post a Comment