KUNA mambo mengi yaliyojificha nyuma ya pazia kufuatia mauaji ya viongozi wa dini ya Kiislam nchini Kenya katika Pwani ya Mombasa, kifo cha Kiongozi na Muhubiri wa dini ya Kiislamu Abubakar Sheikh Shariff maarufu kama Makaburi imeweza kuibua mambo mengi yanayotajwa kuwa chanzo cha mauaji ya kutisha na kinyama katika eneo hilo.
Moja ya Sababu inayotajwa kuwa ni chanzo cha mauaji hayo ni suala la ushiriki wao katika masuala mbalimbali ya kigaidi yanayohusishwa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab cha nchini Somalia, Hata hivyo Serikali ya Kenya tayari imekana kuhusika na mauaji ya kiongozi huyo huku Serikali ikiahidi kufanya uchunguzi wa kina na kuwatambua wauaji.
Kauli hiyo ya Serikali pengine imezidisha hasira ya wafuasi wa kiongozi huo katika pwani ya Mombasa ambao wamekuwa wakiandamana kupinga mauaji hayo, sababu kubwa inayowafanya wafuasi hao kupinga kauli ya Serikali badala yake wamekuwa wakiishutumu Serikali kwamba imehusika katika matukio hayo, inatokana na historia ya mauaji ya viongozi wa dini yaliowahi kutokea nchini humo kwa siku za nyumba.
Duru za ndani kutoka msikiti wa Mussa mjini Mombasa zinadai kwamba Serikali imekuwa ikitekeleza mauaji ya viongozi wa Kiislamu katika maeneo hayo kutokana na shinikizo la Serikali ya Marekani. Akizungumza na Habarimpya.com mjini Mombasa mmoja wa viongozi wa juu katika msikiti huo alisema kwamba Vigogo wa Serikali ya Marekani wamekuwa wakiishinikiza Serikali ya Kenya kuhusu mauaji ya viongozi hao baada ya kubainika kwamba wakifikishwa Mahakama wanashinda kesi zao kutokana na Serikali kukosa ushahidi kamili wa kuwatia hatiani.
Kiongozi huyo ambaye aligoma kutaja jina lake mtandaoni kwa kuhofia usalama wake alisema kwamba sababu nyingine ambayo bado haijatajwa wazi kuhusu chuki ya Serikali na viogozi wa dini katika ukanda wa Pwani ya Mombasa, inatokana na suala la viongozi hao kupingana na Serikali ya Kenya hasa pale ambapo wananchi wa eneo hilo wanapojaribu kuhoji uhalali wa Serikali kushindwa kupeleka huduma za kijamii katika eneo hilo.
."Serikali ya Kenya imekuwa ikipinga hatua ya viongozi wa dini kuwasaidia wananchi katika Pwani ya Mombasa, kwa madai kwamba viomgozi hao wanampango wa kuigawa Kenya na kuitangaza ukanda huo kama Jamhuri, hii ni moja ya sababu iliyofanya Serikali kuongeza chuki ya kidini katika eneo hili, suala lingine ni shinikizo la Serikali ya Marekani kwani mara kadhaa wamekuwa wakiishinikiza Serikali ya Kenya kufanya mauaji"alisema kiongozi huyo wa dini.
Haya ni mauaji ya tatu kutekelezwa katika Pwani ya Mombasa nchini Kenya, yakihusisha viongozi wa dini ya Kiislamu huku serikali ikituhumiwa kutekeleza mauaji hayo inaelezwa kwamba Makaburi alikuwa ni rafiki mkubwa na marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa katika mazingira yanayofanana na hayo.
Kabla ya mauaji ya Makaburi iliwahi kutokea jaribio la mauaji ya Sheikh Ahmed Ali Bahero . Bahero ambaye amekuwa akipinga baadhi ya mafundisho ya marehemu Rogo hatua ambayo inaelezwa kwamba amekuwa pandikizi la Serikali kwa nia ya kuvuruga mipango na mikakati ya Makaburi na wafuasi wake.
Makaburi, marehemu Sheikh Rogo na Ibrahim Amur, ambao wote walikuwa wanaohusishwa na ugaidi na mafunzo ya Al -Shabaab na ajira, huku akidaiwa kuvuruga mipango yote ya viongozi wenzao waliojaribu kuwapinga katika maamuzi yao huku akimfanya Kadhi Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya na Maimamu wengine kuishi kwa hofu ya kuuawa na wafuasi wa Rogo.
SOURCE:HABARIMPYA KUPITIA MTANDA BLOG
0 comments :
Post a Comment