Uuzaji
huo umetokana na ongezeko la maradhi ya figo miongoni mwa Watanzania
kwani takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna
wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa
na wanahitaji upandikizaji
Katika
kile kinachoonekana kukithiri kwa hali ngumu ya maisha, baadhi ya
Watanzania wameanza biashara ya kuuza figo zao kwa gharama kubwa kwa
watu wenye mahitaji ya kiungo hicho muhimu mwilini.
Uuzaji
huo umetokana na ongezeko la maradhi ya figo miongoni mwa Watanzania
kwani takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna
wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa
na wanahitaji upandikizaji. Katika uchunguzi wake, mwandishi wa gazeti
hili alifanya kazi ya kutafuta kama wafanyavyo watu wengine wenye
mahitaji hayo na alifanikiwa kukutana na watu kadhaa ambao walikuwa
tayari kumwuzia lakini kwa gharama kubwa.
Kijana
mmoja alikuwa tayari kumwuzia figo mwandishi wetu. Katika kufikia
makubaliano mazungumzo ya kijana huyo, Abiyudi Mtaki na mwandishi wetu
yalikuwa hivi:
Mwandishi: “Habari
yako kaka, nimepata namba yako kutoka kwa (jina linahifadhiwa) amesema
upo tayari kuuza figo yako, mimi nina shida kwa sababu mama yangu
anahitaji na hali yake si nzuri.”
Muuzaji: “Nitumie meseji nipo kwenye gari.”
Alipotumiwa
meseji alijibu hivi: “Dada yangu mimi naelekea Uganda, kuna mtu
kanitumia tiketi jana, wakala nilimwambia kuwa nauza, ila yeye
hakuniambia iwapo kuna mtu wa Dar es Salaam anayehitaji.”
Mwandishi: “Jamani kaka tusaidie kwa sababu tuna shida, kwani huyo wa Uganda anakupa shilingi ngapi?”
Muuzaji: “Napata milioni 80 aisee!”
Mwandishi: “Basi sitaweza kupata hizo fedha, ngoja niangalie namna nyingine.”
Muuzaji: “Kwani we ulikuwa na ngapi?”
Mwandishi: “Tuna shilingi milioni 20 tu.”
Kiwango hicho hakikukubaliwa na muuzaji huyo.
-MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment