Hii haiwezi kuhitimisha tetesi
za David De Gea kujiunga na Real Madrid majira haya ya kiangazi, lakini
inatia moyo kwa kiasi kikubwa hususani kwa mashabiki wa Manchester
United.
Leo Gazeti la Marca (tazama
picha chini) limekuja na stori kwenye ukurasa wake wa Mbele ikiwa na
picha ya David De Gea na Bosi wa Manchester United, Lois van Gaal yenye
kichwa cha habari “Siempre Negativo” – “Always Negative”.
De Gea amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Man United na kwa miezi mingi amekuwa akihusishwa kutua Real Madrid.
Marca wameripoti kwamba Louis
van Gaal anajitahidi kadri awezavyo kuzuia mpango wa Real Madrid
kumsajili golikipa huyo namba moja Old Trafford.
Gazeti hilo linasema kwamba
kutokana na ugumu uliopo , Real Madrid wameshaanza kuangalia mpango wa
pili ambao ni kumsajili kipa wa Leverkusen, Bernd Leno ili kurithi
mikoba ya Casillas.
Marca mara zote wamekuwa kama
wasemaji wa Real Madrid, lakini sasa inashangaza kwa taarifa hiyo hasi
waliyochapisha kuhusu miamba ya Bernabeu, tena ukurasa wa mbele.
Habari hizi ni nzuri kwa mashabiki wa Manchester United;
0 comments :
Post a Comment