MESSI AWASILI GABON NA KUPEWA HESHIMA KUBWA
Aweka jiwe la msingi AFCON 2017 Gabon
Mchezaji bora wa dunia mara nne, Lionel Messi amewasili barani Afrika na kupewa heshima ya kuweka jiwe la msingi kwenye uwanja yatakapofanyika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 nchini Gabon.
Akiwa amevalia kaptula ya jinzi zinazopendwa na vijana, fulana nyeupe yenye picha aliungana na Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba na maofisa wengine waliokuwa katika mavazi rasmi na kuweka jiwe hilo la msingi.
Messi aliwaongoza Barcelona kutwaa mataji matatu msimu uliopita – ubingwa wa Hispania, Kombe la Mfalme na Ubingwa wa Ulaya aliianzisha rasmi kazi ya ujenzi katika uwanja wa Port-Gentil utakaotumika kwa mechi hizo za 2017.
Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika kwenye eneo kubwa lenye mchanga ambako uwanja husika utajengwa. Hii ilikuwa safari ya kwanza kwa Messi kufika nchini Gabon, ambapo pamoja na mambo mengine alitia saini yake kwenye vitu mbalimbali alivyoombwa, ikiwa ni pamoja na jezi za washabiki wake wanazovaa.
Rais Ondimba alitoboa siri kwamba alikutana na Messi jijini Barcelona miaka michache iliyopita na kumwambia kwamba angefika jijini Libreville kutembea na sasa anaona fahari kwamba mtu maarufu kama Messi ameitimiza ahadi hiyo, hivyo akamrejea kama mtu mwenye heshima.
Uwanja huo mpya utachukua washabiki 20,000 na unatarajiwa kutumiwa kwa ajili ya mechi mbalimbali kuanzia Novemba mwakani kuelekea kwenye michuano hiyo. Port Gentil ni jiji la pili kwa ukubwa nchini Gabon baada ya Libreville.
Michuano hiyo mikubwa zaidi barani itashirikisha timu 16 za mataifa mbalimbali, Gabon wakiwa tayari wamepitishwa kwa sababuya uenyeji. Tanzania walishatolewakatika hatua za awali.
0 comments :
Post a Comment