-->

LEO JULAI 21 ZITTO KABWE KUMKABIDHI MOSES MACHALI KADI YA ACT WAZALENDO


Kiongozi  wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, leo julai 21 atampokea Mbunge wa Kasulu, mjini Moses Machali(NCCR-Mageuzi), ambaye  atatambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.
 
Kwa mujibu wa  taarifa iliyotolewa jana na  Abdallah Khamis Afisa Habari -ACT-Wazalendo  imesema  kwamba   Machali ataambatana na Madiwani wawili,Kamishna wa mkoa mmoja na katibu wake pamoja na wenyeviti na makatibu wa kata 12 zilizo katika jimbo la Kasulu mjini.
 
Katika mapokezi hayo kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe atawapokea na makatibu uenezi 9 wa jimbo la Kasulu mjini yenye jumla ya kata 15 za uchaguzi .
 
Mbali na viongozi hao wengine watakaoambatana na Machali kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo siku ya jumanne julai 21/2015 ni pamoja na wenyeviti wa matawi 101 na makatibu 98, watakaoambatana na wanachama wa awali 648.
 
Wanachama na viongozi wote hao wanatoka katika Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Kasulu mjini.
 
Baada ya Mapokezi hayo ya wanachama wapya wa ACT Wazalendo, Kiongozi wa Chama Zitto Kabwe ataelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapokea viongozi na madiwani kutoka vyama mbali mbali zoezi litakalofanyika siku ya jumamosi julai 25.
 
Julai 26 Kiongozi wa Chama atakutana na watia azma wa nafasi ya Ubunge katika majimbo ya jiji la Dar esSalaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi .
 
Wakati kiongozi wa Chama akiwa mikoani kwa ajili ya kuwapokea wanachama wapya, jijini Dar esSalaam siku ya jumatano julai 22 viongozi wengine watakuwa na jukumu la kuwapokea wanachama na waliokuwa madiwani katika vvama tofauti.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment