-->

ACT WAZALENDO KUMTANGAZA MGOMBEA WAO WA URAISI AGOSTI 10


Zitto Kabwe
Leo siku nzima nilikuwa nina kikao cha mashauriano na Viongozi wa chama wa kata zote za mkoa wa Dar es Salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya Dar) . Jumla ya wajumbe 1023 walihudhuria.
Tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA. Ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya Chama ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki. Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA. Sisi tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe. Tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais tutakayemwunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT Wazalendo.
Tutanadi ‪#‎AzimioLaTabora‬ kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment