Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza kutoa zawadi ya shilingi za kitanzania million 50 kwa mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika na za haraka zitakazofanikisha kuwakamata wote waliovamia kituo cha polisi stakishari na kuua askari na raia waliokuwa katika kituo hicho usiku wa kuamkia jana.
Akitoa tarifa mbele ya wanahabari kamishna wa polisi kanda maalum ya
Dar es Salaam Suleimani Kova amesema kuwa kupitia dhana ya polisi ya
ulinzi shirikishi mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu ameona ni
muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika suala hili
linalohusiana na ulinzi na usalama wao na watanzania wote kwa ujumla.
Jeshi hilo limesema kwamba Mtu yeyote atakaye atakayefanikisha
kukamatwa ikiwemo kutoa taarifa sahihi kwa viongozi wakuu wa jeshi la
polisi atajipatia zawadi hiyo bila hiyana.
Namba za kupiga kama unazo taarifa sahihi ni hizi zifuatazo;
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM (CPS.H KOVA) —–0754034224
MSEMAJI WA JUESHI LA POLISI (SSP ADVERA BULIMBA)—–0713631667
MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI (CP DIWANI ATHMAN)—-0715323444
Aidha wananchi wenye taarifa husika pia wanaweza kuonana uso nkwa uso
na viongozi wakuu wa makao makuu ya polisi au kanda maalum na kuwapa
taarifa moja kwa moja
Jeshi hilo limesisitiza kuwa mwananchi ambaye ataleta taarifa
husika na kufanikisha zoezi hilo itakuwa siri kubwa na hatajulikana
popote kama yeye ndiye mtoa taarifa husika.
Mpekuzi blog
0 comments :
Post a Comment