-->

RONALDO AKERWA NA BENITEZ MAZOEZINI

angry-cristiano-ronaldo-unhappy
Media mbalimbali zimekua zikifuatilia uhusiano wa Cristiano Ronaldo na kocha Benitez kutokana na kwamba ushawishi mkubwa ambao Ronaldo anao ndani na nje ya timu.
Kama una hamu ya kujua kiasi gani Cristiano Ronaldo anapenda kufunga magoli, basi hapa umepata jibu.
Real Madrid wanaendelea na maandalizi ya msimu mpya huko Australia na sasa wanajiandaa kucheza mechi ya kirafiki ya michuano ya International Champions Cup itayopigwa Ijumaa dhidi ya Manchester City.
Kuna video moja imeonekana leo kwenye chombo kimoja cha Hispania ikimuonesha Ronaldo akimuwakia kocha mkuu wa klabu hiyo Rafa Benitez baada ya kukataa goli lake. Baadhi ya vyombo vya habari vimejaribu kufuatilia alichokua anakisema Ronaldo kwa kutafsiri jinsi lips zake zinavyoenda na majibu ni kwamba hakupenda kilichotokea.
Vyombo vingine vinasema ni kawaida kwa mchezaji yoyote hawezi kufurai pale ambapo goli lake limekataliwa na mwamuzi wa mchezo. Hivyo ni kawaida kwa Ronaldo kukasirika baada ya goli lake kukataliwa. Haimaanishi kwamba wana matatizo yoyote kati yao
Angalia video hapa chini:


Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment