Wakati leo saa 10 jioni ndiyo muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania Urais ndani ya CHADEMA, hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua.
Hali hiyo inazidisha sintofahamu iliyougubika mchakato wa Urais ndani ya chama hicho na ndani ya UKAWA, kuwa huenda kuna ‘mtu wa nne’ anayesubiriwa kutoka nje ya chama hicho japo kuhusu Viongozi na Wabunge wa chama hicho walisema Edward Lowassaanakaribishwa mradi tu afuate kanuni na taratibu.
Suala la mgombea Urais wa UKAWA limeendelea kuteka mjadala wa kisiasa nchini huku Watanzania wakisubiri kufahamu nani atateuliwa kupambana na Mgombea wa CCM, Dk. John Magufuli.
Katika Mkutano wake uliofanyika Mwanza Jumatano Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwaomba Watanzania wavumilie wakati wanakamilisha taratibu za kumpata mgombea Urais.
Pia, ilielezwa kuwa chama hicho kilikuwa kinasubiri mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF unaofanyika leo, huku taarifa nyingine zikisema chama hicho kilikuwa hakijampata mgombea mwenza kutoka Zanzibar.
Ratiba ya kuchukua fomu za Urais na kurudisha ilikuwa inaonyesha ni leo na hakukuwa na dalili zinazoonesha watu kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema kuna marekebisho yamefanyika katika tarehe hiyo ya mwisho kurejesha fomu ambayo yatatangazwa ndani ya siku mbili au tatu ambayo yalilenga kupisha mchakato wa kura za maoni, baadae chama hicho kilitoa taarifa ya kusogeza mbele tarehe ya kurudisha fomu hadi Julai 31, 2015 saa 10 jioni.
0 comments :
Post a Comment