Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja
viwili vya Taifa na Karume vilivyopo jijini Dar es salaam, itaendelea
kesho kwa michezo miwili itayopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Katika
michezo iliyochezwa leo, Malakia ya Sudani Kusini iliibuka na ushindi
wa mabao 2- 1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia, LLB ya Burundi ikitoka
sare ya bila kufungana na Heegan FC ya Somalia mchezo uliochezwa saa
uwanja wa Karume, huku Azam FC wakiibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya
KCCA ya Uganda.
Vinara wa kundi A timu ya Gor Mahia kutoka nchini
Kenya, kesho jumatatu watashuka dimbani kucheza na timu ya KMKM kutoka
Visiwani Zanzibar ambayo pia jana iliibuka na ushindi katika mchezo wake
wa awali dhidi ya Telecom.
Gor Mahia ambayo ilipata ushindi wa
mabao 2- 1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, itakutana na KMKM
ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya timu ya Telecom ya
Djibout, mchezo utakaochezwa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Mchezo
wa kwanza utazikutanisha timu za Telecom ya Djibout dhidi ya Khartoum-3
kutoka nchini Sudan, ambayo itakua ikicheza mchezo wake wa kwanza.
Jumanne
kutakua na michezo mitatu ambapo Al Shandy watacheza na LLB katika
kundi B saa 8 mchana uwanja wa Taifa, Heegan FC dhidi ya APR uwanja wa
Karume saa 10 jioni, Malakia dhidi ya Azam kundi C Uwanja wa Taifa saa
10 jioni.
Jumatano mabingwa mara tano wa michuano ya Cecafa Kagame
Cup, timu ya Yanga SC watacheza dhidi ya Telecom ya Djibout saa 10
jioni uwanja wa Taifa, KCCA wakicheza na Adama City saa 10 jioni uwanja
wa Karume, na Khartoum wakicheza mchezo wa awali saa 8 mchana uwanja wa
Taifa dhidi ya KMKM.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment