Nakala ambayo yumkini ikawa miongoni mwa nakala za zamani zaidi za kitabu kitakatifu cha Qur'ani Tukufu imegundulwia nchini Uingereza.
Gazeti la Times la Uingereza limeripoti kuwa, uchunguzi uliofanyika katika ngozi ambayo Qur'ani hiyo imeandikwa umethibitisha kuwa mnyama wa ngozi hiyo alikuwa akiishi katika zama za Mtume Muhammad (saw) au muda mfupi baadaye. Prof David Thomas wa Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza ambaye ni mtaalamu wa Uislamu na Ukristo amesema kuwa matokeo ya uchunguzi huo yanashangaza na kwamba nakala hiyo ya Qur'ani ya kale inafanana na Qur'ani iliyopo hivi sasa baina ya Waislamu. Thomas amesema uchunguzi wa Chuo Kikuu cha Oxford umebaini kuwa, kuna uwezekano wa asilimia 95 kwamba nakala hiyo iliandikwa baina ya mwaka 568 hadi 645 Miladia na kwa msingi huo mtu aliyeiandika alikuwa akiishi katika zama za Mtume Muhammad (saw). Profesa huyo amesisitiza kuwa, ugunduzi wa moja kati ya nakala za kale zaidi za Qur'ani umesisimua sana.
0 comments :
Post a Comment