-->

NAPE NAUYE ASEMA MANENO MAZITO YENYE KUCHOMA,BOFYA HAPA KUYASOMA

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejigamba kwamba kimeweza kuzuia ‘mafuriko’ kwa mikono huku kikiwatakia kila la kheri baadhi ya makada wake waliotangaza kutogombea kupitia chama hicho pamoja na wale waliokihama na wanaotaka kukihama.Mwishoni mwa wiki iliyopita waliokuwa madiwani jimbo la Monduli kupitia CCM mkoani Arusha, walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku wabunge wa viti maalum, Ester Bulaya na James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama wakitangaza kutogombea kupitia chama hicho
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na mtandao huu jana alisema CCM hakina uwezo wa kuzuia mtu anayetaka kukihama kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia

SOURCE:THE CHOICE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment