-->

TAARIFA YA KUONEKANA KWA MWEZI

Eid ul-Fitr moon sighted in Saudi Arabia, other countries
Nchini Saudi Arabia wameingia katika mwezi Shawwal na kuanza kusheherekea Eid il fitri sanjari na waislam waliopo nchini Tanzania hasa wale wenye kufungua kwa kuzingatia kigezo cha uonekanapo  mwezi(yaani mahali popote)
Nchini Tanzania mapema baada ya swala ya maghari ya trh 16 viongozi wa BARAZA LA SUNNA(BASUTA)Walitangaza kuonekana kwa mwezi na kuwatangazia waumini wao kusherekea Eid il fitrty.
Nae katibu wa baraza hilo la sunna maarufu kama BASUTA Shekh Mohammed Issa  alisema wamepata taarifa ya kuonekana kwa mwezi pia hapa nchini,huko Dodoma maeneo ya Kondoa.
Tayari viwanja vya kuswaliwa swala hiyo ya Eid vimeshatangazwa katika mikoa tofauti tofauti.
Nae shekh mkuu wa Dar es salaam akikaimu nafasi ya kaimu muft amewatangazia waumini kuwa sherehe za Eid itafanyika jumamosi kwani wao hawajauona mwezi na wala hawana taarifa za kuonekana kwa mwezi.
Pia Channel ya ITV kupitia mtandao wao wa facebook waliandika kuhusu kuingia Eid katika baadhi ya nchi nyingine kama vile Uturuki

#Mudawakutekelezasala ya Eid el Fitr #UturukiiWakati Mwezi wa Ramadhan ukielekea ukingoni huku Waislam Ulimwenguni...
Posted by ITV Tanzania on Thursday, July 16, 2015
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment