Mchezaji wa Manchester United Angel
Di Maria amewaeleza wakuu wa kilabu ya PSG nchini Ufaransa kwamba
anataka kujiunga na kilabu hiyo.
Kulingana na gazeti la Le
Perisien mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yanaendelea huku
wakidaiwa kukubaliana kwa kitita cha pauni milioni 42.8.Di Maria amekosa kuichezea Man United katika ziara ya timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu ujao nchini Marekani akidaiwa kupumzika baada ya kushiriki katika kombe la Copa America.
0 comments :
Post a Comment