Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa
na klabu ya Yanga akitokea Mgambo JKT ya Tanga, Malimi Busungu, leo
amefanikiwa kufunga magoli mawili kati ya matatu wakati Yanga ikicheza
dhidi ya Telecom ya Djibouti kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya Kagame
Cup na kuifanya Yanga kuandika ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo
inayozidi kuchukua sura mpya.
Busungu alianza kufunga goli la
kwanza dakika ya 26 kipindi cha kwanza bada ya mashambulizi kadhaa
hatimaye akafanikiwa kuukwambisha mpira kambani.
Kitu kilichowashangaza mashabikim
wengi wa Yanga ni pale timu hiyo ilipopata penati mbili lakini wapigaji
walishindwa kutumia nafasi hizo kufunga magoli.
Amis Tambwe alikosa penati ya
kwanza dakika ya 36 baada ya Simon Msuva kuangushwa kwenye eneo la
hatari lakini Tambwe alipiga mpira nje. Dakika ya 45 Yanga ilipata
penati baada ya mlini wa Telecom kuunawa mpira kwenye eneo la hatari
lakini Simon Msuva mfungaji bora na mchezaji bora wa ligi msimu uliopita
penati yake ilipanguiliwa na golikipa wa Telecom Nzokira Jeef.
Kipindi cha kwanza kilimalizika
Yanga wakiwa mbele kwa goli 1-0 kitu ambacho kiliwashangaza wengi
kwasababu walikuwa wakiamini Telecom ni timu dhaifu kutokana na kufungwa
goli 5-0 na Khartoum ya Sudan.
Kipindi cha pili kocha wa Yanga
Van Pluijm alifanya mabadiliko kwa kumtoa Simon Msuva na nafasi yake
ikachukuliwa na Godfrey Mwashiuya wakati Amis Tambwe nafasi yake ilichukuliwa na Kpah Sherman na Deus Kaseke alitolewa kumpisha Andrey Coutinho.
Dakika ya 68 Busungu alifunga
goli la pili kabla ya Mwashiuya hajamalizia bao la tatu na lamwisho
dakika ya 74 akipiga shuti kali lililogonga mtambaa panya kisha kumgonga
mlinda mlango na kutinga nyavuni.
Baada ya mchezo kumalizika,
Malimi Busungu alaitangazwa kuwa nyota wa mchezo huo na kukabidhiwa
king’amuzi na kituo cha television cha DSTV.
Kwa
matokeo hayo, Gor Mahia wanaendelea kuongoza kundi A wakiwa na pointi
6, wakifuatiwa na Khartoum ambayo inapointi sita pia lakini
wanatofautiana magoli ya kufunga na kufungwa. Yanga wapo nafasi ya tatu
wakiwa na pointi tatu sawa na KMKM lakini nao
wanatofautihwa kwa maoli na Telecom ndio wanashika mkia kwenye kundi
hilo wakiwa hawajapata ponti hata moja.
0 comments :
Post a Comment