-->

SCHWEINSTEIGER KUIKOSA MECHI YA BARCELONA NA MANCHESTER UNTED BAADA YA KUUMIA

Louis van Gaal has confirmed Bastian Schweinsteiger will miss Manchester United's clash with Barcelona
Bastian Schweinsteiger hatacheza katika mchezo wa kirafiki wa Manchester United dhidi ya Barcelona kuwania taji la International Champions Cup baada ya kiungo huyo wa Ujerumani kuumia. Schweinsteiger ambaye ametua Old Trafford kwa dili la pauni milioni 15 akitokea Bayern Munich mapema mwezi huu, alicheza mchezo wake wa kwanza kwa Manchester United Jumanne iliyopita dhidi ya San Jose Earthquakes. Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema: "Schweinsteiger hatacheza Jumamosi kwa sababu ameumia kidogo na sitapenda kucheza kamari juu ya hilo." Van Gaal amesema safari hii huenda wachezaji 11 wa mwanzo wakacheza kwa dakika 60 na wale wa pili wakamalizia dakika 30 tofauti na mechi mbili zilizopita ambapo alikuwa akibadili kikosi kizima wakati wa mapumziko. Louis van Gaal has confirmed Bastian Schweinsteiger will miss Manchester United's clash with Barcelona Louis van Gaal amethibitisha kuwa Bastian Schweinsteiger ataukosa mchezo dhidi ya Barcelona Bastian Schweinsteiger ameumia kidogo
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment