-->

BABA NA MWANA(RIVALDO NA RIVALDINHO) WATUPIA MAGOLI TIMU YAO IKISHINDA BAO 3 KWA 1

video-undefined-1BA1565700000578-376 636x358LEJENDARI wa Brazil, Rivaldo, ambae alitwaa Kombe la Dunia Mwaka 2002, na Mtoto wake Rivaldinho wote walipiga Bao walipoichezea Mogi Mirim ilipoifunga Macae 3-1 katika Mechi ya Daraja la Pili huko Brazil.
Rivaldo, mwenye Miaka 43, alichangia Bao zote 3 za Timu yake likiwamo lile la Krosi yake ya Dakika ya 3 tu kuunganishwa kwa Kichwa na Mwanawe Rivaldinho, mwenye Miaka 20.
Rivaldo, ambae aliwahi pia kuzichezea Klabu za Barcelona na AC Milan, alifunga Bao lake kwenye Mechi hiyo kwa Penati.
Lejendari huyo wa Brazil alistaafu Soka Machi 2014 lakini mapema Mwezi huu akaamua kurejea tena Uwanjani.
Kwenye Dunia ya Soka ishawahi kutokea Baba na Mwana kuwa Wachezaji kwa wakati mmoja, kama vile Familia ya Clough na Maldini, lakini ni wachache waliowahi kucheza pamoja. 
Huko England, Ian Bower, aliewahi kutwaa Kombe la Ulaya, aliwahi kucheza na Mwanawe Gary wakiwa Hereford United wakati Alec Herd, aliewahi kuichezea Man City, alicheza pamoja na Mwanawe David, ambae baadae alienda Man United, wakiwa Stockport County katika Miaka ya 1950.
Mwaka 1966, Eidur Gudjohnsen, aliewahi kuichezea Chelsea, akiwa na Miaka  17, aliingizwa kutoka Benchi kumbadili Baba yake Arnor, aliekuwa na Miaka 34, wakati Nchi yao Iceland ilipoichapa Estonia 3-0 lakini wawili hao hawakuwahi kucheza Klabu moja.
Tanzania Je ishawahi kutokea hii? Au itatokea?
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment