Maelfu ya wakazi wa Zanzibar wamempokea mgombea urais kupitia CCM, Dk Magufuli na makamu wake Samia Suluhu wakati wa mapokezi eneo la Kwenye Bao la Kachorora.
Dk Magufuli ambaye ni waziri wa ujenzi ataungana na mgombea mwenza kutoka wizara ya nchi, ofisi ya makamu wa rais (Muungano) tayari amewaaga na kuwashuru wafanyakazi wenzake katika ofisi hiyo ya makamu wa rais.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.
Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kushuhudia sherehe fupi za kutambulishwa kwa wagombea wa nafasi ya Urais kwa kupitia CCM kwenye viwanja vya Afisi Kuu.Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Mhe. Hassan Suluhu Hassan akizungumza kwenye sherehe fupi za utambulisho nje ya Afisi kuu ya CCM Zanzibar.Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akiwasalimu wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye sherehe za kumtambulisha yeye na mgombea mweza kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar.Wakazi wa Zanzibar wakimsikiliza mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgombea wa ueais kwa kupitia CCM Dk.John Magufuli.
0 comments :
Post a Comment