msunga
Bw. Jumanne Juma Msunga.
Na Hillary Shoo, SINGIDA
MSAIDIZI  wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama  CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake.
Akitangaza uamuzi wake huo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA  Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA,huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.
Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.
“Kuna viongozi  wakuu wa nchi hii ambao mimi nawaheshimu kama vile Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Makamu wa Rais Mohamed Bilal, Edward Lowassa hawakunusa hata tano bora, hiyo sio haki ni dhuluma tu ilifanyika kwa maslahi ya mtu mmoja, kwa hiyo mimi kama kijana nimeona nifanye maamuzi magumu ya kuondoka ndani ya CCM.” Alisistiza Msunga.
Hata hivyo alisema haina maana kuendele kuwa amwajiriwa wa chama ambacho hakitendi haki na hivyo anaamini kwa kijunga kwake CHADEMA kumempatia faraja kwani anajisikia kuwa huru sasa.
“Vijana wenzangu huu ni wakati wa fungukeni sasa jiungeni na CHADEMA ni chama cha nguvu ya umma na mara zote haki itatendeka huku kwani nimekuwa kiongozi ndani ya CCM toka mwaka 2012 na ni mtumishi hadi leo hii na hata ofisi yao bado sijaikabidhi”,  alisema.
ofisi