WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi
la Katavi la kumtaka
agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.
agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa
Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili, Julai 19, 2015), Waziri
Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia
Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa
yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati
wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu
katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze
kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la Katavi wawe makini
katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu
wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya
wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi aliwaasa wananchi wa Wilaya ya
Mlele kumuenzi Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hata atakapokuwa
amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea
maendeleo.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.
0 comments :
Post a Comment