-->

MAKALA MPYA KUSUHUSU VIDONDA VYA TUMBO PAMOJA NA TIBA YAKE

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea endapo kidonda cha ukubwa wa angalau nusu sentimeta kitatokea kwenye sehemu yoyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili husababisha maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu makali ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa karibu 70% - 90% ya vidonda vya tumbo husababishwa na vimelea vya bakteria wajulikanao kama HELICOBACTER PYLORI. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-Inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama Duodenum.

AINA YA VIDONDA VYA TUMBO.
1. Vidonda vinavyotokea katika mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Vidonda hivi hujulikana kama Gastric Ulcers.
2. Vidonda vinavyotokea katika sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo. Vidonda hivi hujulikana kwa kitaalamu kama Duodenal Ulcers.
3. Vidonda vinavyotokea katika koo (Oesophageal Ulcers)
4. Vidonda aina ya Merckel's Diverticulum Ulcers. Vidonda vya aina hii huweza kusababisha matatizo makubwa ya utumbo (intestinal obstructions)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
1. Maambukizi ya Bakteria aina ya Helicobacter pylor. Imeonekana kuwa zaidi ya 50% ya watu Duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao huwa hawaonyeshi dalili yoyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
2. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs. Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikanavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa utengenezaji vichocheo hivi yaani Prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.
3. Vyakula au viungo vya vyakula vyenye uchachu. Kinyume na ilivyozoeleka kwa wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.
4. Uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylor huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike kuwa uvutaji wa sigara pekee hautoshi kusababisha vidonda vya tumbo isipokuwa kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor.
5. Watu walio katika kundi la damu la O. Imeonekana pia kwamba kundi la damu la BLOOD GROUP O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.
6. Unywaji wa pombe. Unywaji wa pombe kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor huongeza madhara ya vidonda vya tumbo.
Vitu vingine vinavyohusishwa na uongezaji wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni pamoja na Upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeris), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo na kubadilishiwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
-Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastric pains).
-Maumivu makali kipindi cha kula au baada ya kula.
-Maumivu makali wakati unapokuwa na njaa.
-Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii yaweza kuendana pamoja na kubeua au kujamba mara kwa mara.
-Kucheua au kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumbomi baada ya kucheua.
-Kichefuchefu na kutapika.
-Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.
-Kutapika damu.
-Kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha kuwa mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali.
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia  dawa za kupunguza maumivu NSAIDs kwa muda mrefu bila kufuata ushauri wa Daktari ni ishara moja ya kumfanya mgonjwa kumuona Daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Mara nyingi mchanganyiko wa dawa za Antibiotics mbili hasa Amoxyllin + Metronidazole sambamba na dawa yoyote ya jamii ya PPI kama Pantoprazole au Omeprazole. Hiyo ni kwa mgonjwa wa vidonda ambavyo siyo sugu.
Vidonda sugu inampasa mgonjwa kutumia dawa za antibiotics za aina tatu kama Amoxyllin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yoyote moja kutoka kundi la PPI kama Omeprazole na Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.

Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bakteria, dawa yoyote moja ya jamii ya PPI yaweza kutumika kwa muda mrefu bila kuchanganya na antibiotic yoyote.
Hata hivyo inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia, hivyo ni vyema kuhakikisha unapata matibabu sahihi na uhakikishe unamaliza dozi kwa muda sahihi. Kumekuwa na watu wengi kuanza matibabu vizuri lakini huishia njiani na kutomaliza dozi. Huu siyo ugonjwa mdogo kwamba utumie dawa kwa siku tatu au wiki moja kisha unapona, huu ni ugonjwa sugu hivyo matibabu yake pia ni ya muda mrefu kidogo kutegemeana na aina ya dawa unazotumia.
Dawa iliyotengenezwa kwa mmea wa Mwalovera imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wote wa vidonda vya tumbo. Hutibu kabisa vidonda vya tumbo kwa kuwaangamiza kabisa bakteria wote wasiofaa katika tumbo. Dozi tatu za dawa hii kwa muda wa miezi mitatu humaliza kabisa ugonjwa huu.
=>Kuipata dawa hii wasiliana nasi kwa 0767925000 au 0784925000 utaweza kuipata mahali popote ulipo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment