Written By Boaz Mkumbo on Sunday, October 11, 2015 | 3:58 AM
HATUA TANO ZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME KATIKA NDOA YAKO
Napenda kukukaribisha tena katika jukwaa langu la afya yako,
leo hii napenda nizungumzie tatizo ambalo limekuwa ni kubwa sana kupita kiasi
kwa kila m, tatizo ambalo linayumbisha na kuweka ndoa matatani, usiwe miongoni
mwa watu wenye upungufu wa nguvu za kiume, yote hayo utayaepuka kwa kufuata
ushauri huu ulio badili maisha ya watu wengi na bado elimu hii inaendelea kutoa
shuhuda kwa kila mtu aliyekuwa na tatizo hili.
Nguvu za kiume hapo zamani za kale na tafiti za kisayansi
zinaonesha ni matokeo yanayotokea uzeeni kuwa ni jambo la kawaida kwa umri
mkubwa, lakini napenda nikwambie kuwa uzeeni ambao unaambatana na magonjwa sugu
kiasi hicho ni moja wapo ya sababu nikuweke kwenye kundi la watu wanaozeeka
vibaya. Kwa kawaida binadamu hustahili kuzeeka na magonjwa tunazeeka na
magonjwa kwa sababu tunayasababisha sisi
kwa maisha ya kifahari tunayoishi na
kusahau kuwa afya yako sio hazina ya milele,unatakiwa kuiheshimu,kuilinda na
kuimarisha ili uje ufurahie uzee wako usio na magonjwa. Najua kuwa hadi sasa
ukifanya tafiti vijana wa umri wa miaka 20 hadi 30 ndio wanao ongoza kwa
kusumbuka na matatizo haya ya nguvu za kiume tofauti na matarajio yetu wote
kuwa tatizo hili tunasoma kuwa linawapata wazee, swali la kujiuliza kwa nini
sasa vijana tena katika umri mdogo? Ndio maana nimeamua kukuandikia Makala hii
ambapo kama ni miongoni mwa watu wanaosumbuka hili tatizo nina uhakika tatizo
lako utapata suluhisho kutokana na elimu hii rafiki yangu. Pia najua unaweza
ukawa na mchumba wako, unavumulia mengi kuhusu tatizo hili la mwenzi wako,
usiwe mkimya kwani inahitaji utashi wa juu sana kumweleza mwenzi wako kuhusu
hili swala kwani upungufu wa nguvu za kiume unasababisha msongo wa mawazo
wengine hupelekea hadi kuchanganyikiwa hatimaye kupata MAJOR DEPRESSIVE
DISORDER na mbali na hivyo husababisha kutokujiamini na woga wa kuwa na mke na
hivyo wengi wamejaa wasiwasi na hofu kubwa ya kugunduliwa na mwezi wake kuwa
ana tatizo hilo, na wengi wao ni woga sana kutogunduliwa tatizo hilo,ndio maana
inapofikia hatua mwenza wako umembaini ni mara chache sana atakubali kuwa kweli
ana tatizo hilo. Kwa nini usumbuke na matatizo kama haya wakati msaada wako
upo? Usiendelee kusumbuka na tatizo hili kwani umeumbiwa maisha ya furaha na
Mungu ni haki yako kufurahia uumbaji wa Mungu, anza leo kushughurikia tatizo
kabla halijawa sugu mpendwa msomaji wa Makala hii.
NINI KISABABISHI MSINGI WA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?
Katika mwili wa binadamu kuna vichocheo aina ya Testosterone
ambavyo hutolewa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa ubongo,ufanye kazi
katika hali tulivu,kuondoa,kuondoa msongo,kuondoa mstuko wa aina yoyote
,kuimarisha uwezo wa kufikiri,kuimarisha furaha ya mwili wako na hatimaye
kuimarisha nguvu za kiume na hatimaye kufurahia tendo la ndoa. Kazi kubwa ya
kichecheo hiki ni kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali tulivu kabisa kwa
kuutuliza ubongo wako ndipo utafurahia ndoa yako rafiki yangu.
Sasa endapo kichecheo hiki kikivurugika kinasababisha vichocheo
vingine kama insulin,leptin,cortisol,vichocheo vya ukuaji pia kuvurugika kwani
matokeo ya hitililafu hii mwilini inasababisha
KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME kwa sababu vichocheo hivi vinafanya kazi kwa
ushirikiano mkubwa, na endapo kimoja tu kikivurugika vyote vinapoteza mwelekeo
na tatizo kuwa sugu Zaidi.
Napenda leo nieleze kwa kina kidogo namna gani nguvu za
kiume zinapotea kutokana na mvurugiko wa vichocheo hivyo vikuu vitatu kama
nilivyo vitaja hapo juu.
1.
TESTOSTERONE
Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume
kwani ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe na sifa zote za kiume na ndicho
kicheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa. Upungufu wa kicheo
hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti,kupungua kwa nguvu
za misuli yako kiutendaji,mafuta kurundikana ovyo mwilini( BELLY FAT AND
OBESITY)
Lakini pia ijulikane kuwa kichocheo hiki
cha testosterone sio kwamba kinapatikana kwa wanaume tu, la hasha! Kichocheo
hiki hata wanawake wanacho ingawaje kwa kiwango cha chini sana, endapo
kinapokuwa kimepungua kinaweza kumsababishia mwanamke kukosa matamanio kwa
jinsia ya kiume wakati wa tendo la ndoa, kukosa nguvu ya misuli ya kuhimili
tendo la ndoa (Kuchoka Sana),kuongezeka uzito kupita kiasi na nyama uzembe pia
kupunguza uwezo wako katika kufikiri na kumbu kumbu.
NINI KINASHUSHA TESTOSTERONE MWILINI MWAKO?
Moja ya kisababishi kikubwa cha testosterone
kushuka kiwango chake ni kwa sababu ya kuwepo na kizuizi cha insulin (insulin
resistance) hii inafanya kiwango cha insulin kuwa juu sana na kusababisha
testosterone kushuka kiwango chake. Moja ya sababu zinazo sababisha kiwango cha
insulini kuwa juu sana ni unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na
pia ulaji wa vyakula vyenye vionjo mbalimbali vitamu vilivyotengenezwa
viwandani. Hivyo basi sukari inapokuwa ipo katika kiwango cha juu sana kwenye
damu inasababisha utolewaji wa insulin kuwa katika kiwango cha juu pia kwenda
kusawazisha sukari irudi kawaida. Hivyo basi matumizi ya vyakula na vinywaji
vya sukari nyingi vinafanya mwili upate kizuizi katika utendaji kazi wa insulin
na hatimaye testosterone pia kushuka kiwango chake. Najua umejifunza sasa kwa
nini watu wanaotumia vyakula vya viwandani,vinywaji vya sukari nyingi,ulaji wa
vyakula vyenye mafuta mabaya jinsi gani inasababisha vichocheo vyako kushuka
kiwango na unaendelea kusumbuka sana. Napenda kukuambiwa kuwa siku zote watu
hawaogopi vyakula vyenye sukari wanaogopa vyakula vyenye mafuta mengi, hio ni
fikra potofu sana! Sugar is more addictive than heroin and cocaine, kwa maana
nyingine watu ni walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari na haipo siku anaweza
kuacha haraka. Usihofu kama una tatizo hilo ujue tayari umeshaathiriwa na ulaji
wa vyakula na vinywaji hivyo.
2.
INSULINI
Hiki ni kichecheo ambacho hutolewa na
kongosho lako ili kwenda kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi
kubwa wa maji haya ya insulin ni kuhifadhi nishati ya mwili kwa matumizi ya
baadae pale mwili unapokuwa una nishati ya kutosha na hautaki kupoteza nishati
ya ziada. Nishati hii huhifadhiwa asilimia kubwa katika mfumo wa glycojeni mwilini mwako kwenye
misuli,ini nk. Sasa inapotokea kiwango chako cha ulaji wa vyakula vya sukari ni
kikubwa sana ndivyo kiwango kingi cha insulin kitatengenezwa na kumwagwa kwenye
mzunguko wa damu kwenye kuhifadhi sukari ya ziada ambayo haitumiki wakati ule
na hatimaye kusazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi ya insulin sio
kushusha sukari kama wengi tunavyofundishwa darasani! Kwa nini nasema hivi?
Kazi ya insulin ni kuhifadhi nishati ya ziada kwa matumizi ya baadae na hivyo
basi kupungua kwa sukari ni matokeo ya kazi ya insulin mwilini mwako.
HEBU SOMA TAFAKURI HII:
Umeingia katika chumba ambacho umekuta
harufu mbaya sana ya deodorant spray au perfume punde tu utakapo ingia katika
chumba hicho utasumbuka sana na harufu hio kwa muda mfupi na hatimaye unaizoea
na kuona ni harufu ambayo haina madhara wala usumbufu kwako.
Huu mfano utakusaidia kujua kwa nini
tunasema insulin yako imeshindwa kufanya kazi, na umepata kizuizi katika
utendaji kazi wake. Nimesema insulin hutolewa kwa kiwango kikubwa sana
kulingana na kiwango cha sukari mwilini mwako, kiwango hiki kingi cha insulin
kwenye damu kwa muda mrefu inaweza kupelekea insulin kupoteza kazi yake
kiuhalisia. Na pia kitu kingine ambacho kinaweza kupelekea insulin kutofanya
kazi ni vipokea insulin kutoitikia kwa sababu ya mafuta mabaya kuleta kizuizi
katika vipokezi vya insulin. Vitendo vyote hivi viwili vinasababisha kiwango
cha insulin kuwa juu wakati wote na kama
nilivyo eleza mwanzo kuwa kiwango cha insulin kinavyozidi kuwa kingi mwilini
mwako kinashusha vichocheo vya Testosterone ambavyo ndio silaha yako mwanaume.
Hivyo basi ukiangalia katika maelezo haya utagundua kuwa ulaji wa vyakula na
vinywaji vingi vya sukari vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu muda wote
ambapo nacho kinapelekea vichocheo vya kiume kushuka na hatimaye unakumbwa na matatizo
ya kukosa matamanio kwa jinsia tofauti,msongo wa mawazo,misuli kukosa nguvu
muda wote umechoka,uzito kuongezeka kwa kasi sanana wengine hupelekea kumilki
vitambi.
Pia kiwango kingi cha insulin kwa muda
mrefu kwenye damu kinaweza kupelekea kupata nywele usoni kwa wanawake,mwanaume
kuishiwa vinyweleo sehemu kama kifuani,tumboni na maeneo mengine mengi.
3.
LEPTINI
Hiki ni kichocheo cha pekee sana na huwa
napenda sana kukizungumzia kwani kinaonesha jinsi gani binadamu alivyo umbwa
kwa kutumia teknolojia ya uhandisi wa hali ya juu. Hiki ni kichecheo ambacho
kinatengenezwa na seli zinazohifadhi mafuta ambazo zinapatikana kwa wingi
kwenye misuli kazi yake kubwa ni kupeleka ujumbe kwenye ubongo katika kuendesha
hamu yako unapokuwa una chakula mbele yako, na ubongo huitikia kwa kutoa
taarifa ya kutosheka na chakula kwa kujihsi umeshiba na huwezi tena kuendelea
na chakula.
Sasa basi ulaji wa vyakula vingi bila
mpango vyenye sukari nyingi unasababisha seli za kuhifadhi mafuta (FAT CELLS)
kutengeneza kwa wingi leptin ili kwenda kutimiza kazi yake. Kiwango cha insulin
na leptin hupanda kwa pamoja kama mapacha vile. Hivyo hivyo kumbuka tafakuri
ile pale juu ya perfume, itafikia wakati kiwango kingi sana kinasababisha
leptin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ( KUKATA HAMU YA CHAKULA) hivyo
utakuwa una tatizo la kula mlo mkubwa ambao hata siku moja hautosheki na ukitosheka
muda si mrefu unahitaji tena kula. Hawa ndio watu wengi ni wahanga wa muda wote
wanapenda kula vyakula vitamu vitamu tu, hamu haiishi (Sugary addicted,sugar
craving) na wengi huishia kupata matitizo ya kiafya kama kuishiwa nguvu za
kiume,uzito kupita kiasi,kitambi na kuishiwa nguvu kabisa ya misuli yote haya
ni kwa sababu kiwango kingi cha leptin na insulin kinashusha vicheo vyako vya testosterone.
4.
CORTISOL
Hiki ni kichocheo ambacho hutolewa na mwili
pale unapokuwa katika hali yoyote ya mstuko ili kwenda kukabiliana na mtuko
huo.
Mfano labda Dr Boaz Mkumbo nilikuwa
natembea njiani ghafla nikaona nyoka huyo mkubwa chatu. Mwili utastuka sana na
kutoa vichecheo vinavyo enda kupambana na hio hali iliyoshtua mwili wako, mfano
cortisol huenda kuongeza kiwango cha nishati ya mwili (glucose) kwenye damu na
kuwa na nguvu ajabu ya kumkimbia adui yako aliyepo ,mbele yako.
Cortisol pia hutolewa hata kama mwili wako
umekabiliwa na mstuko ndani kwa ndani mfano,sukari mwilini imepungua mwili
unatoa cortisol ambayo kazi yake kubwa ni kubadili ile nishati iliyokuwa
imehifadhiwa katika mfumo wa glycogen kwenye misuli na ini kuwa sukari na
hatimaye kuongeza sukari mwilini mwako.
Sasa tafiti zinasema kwamba,kiwango kingi
cha cortisol kwenye damu kinachosababishwa na msongo,mstuko ndani ya miili yetu
inayo endelea inasababisha LEPTIN kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo.
Na endapo leptin ikishindwa kufanya kazi
yake ipasavyo utakuwa una tatizo la kula sana hasa vyakula na vinywaji vya sukari bila hamu kukata na hatimaye
kusababisha insulin kupanda juu na testosterone kushuka chini na hatimaye
kuishiwa nguvu za kiume,matamanio kwa jinsia tofauti nk.
Hongera sana kwa kuendelea kusoma Makala hii,
hapo juu nilitaka kukueleza tu nini kinatokea endapo unapatwa na upungufu wa
nguvu za kiume kwani wengi mmekuwa mkinipigia simu kutaka kujua kwa nini nguvu
za kiume sasa, basi leo nazani umejifunza kitu, kama hujaungana nami katika
ukurasa wangu facebook hebu bofya like Dr Boaz Mkumbo MD utafurahia Makala zangu
nyingi sana nzuri zimeandaliwa kwa ajili yako.
Basi napenda nikupe vitu vikuu 4 vinavyo angamiza
watu kukosa nguvu za kiume hawa ndio maadui wako wakuu kuhusu tatizo lako hilo
mpendwa, hebu endelea kusoma upate suluhisho lako,ufurahie ndoa yako,
VITU 4 VINAVYO ANGAMIZA NGUVU ZAKO ZA KIUME
NA KUKUACHA MWENYE MSONGO WA MAWAZO NA MPWEKE KATIKA MAHUSIANO AU NDOA YAKO
Hebu basi napenda nikwambie hawa maadui
wako, najua utashangaa kuwa ni maadui ambao kila siku ni marafiki zako, na
hujui kuwa wanaangamiza msingi wa ndoa yako na inaweza kuwa unajua lakini
unayapuuzia haya tunayokufundisha kupitia elimu hii ya afya, huwa napenda
kuwaambia wagonjwa wangu kuwa afya yako ni mali yako sio ya daktari wala
muuguzi wewe ndiye una mamlaka ya afya yako kuiweka sawa au kuidhoofisha. Hivyo napenda kukuambia kuwa afya yako sio
hazina ya milele linda sana afya kuliko vyovyote ulindavyo kwani ndio msingi wa
furaha zote duniani.
1.
Vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda
Hivi
ndio vimekuwa ni vinywaji vya kila siku hasa kwa wafanya kazi, ndio maana wengi
ndio wamekuwa wakisumbuka na matatizo haya ya kiafya kwani wanakula vyakula
huwa napenda kuviita vya chapuchapu, yani anataka soda ya kuvuta muda ili
baadae akale, ndugu yangu nimeongelea jinsi gani sukari nyingi inashusha nguvu
za kiume tena kwa kina Zaidi. Wengine huuliza sasa Dr mimi siwezi kabisa
kujizuia kunywa soda hata masaa tu, kwani kwenye friji zimejaa, ni kweli huwezi
kujizuia kwa sababu tayari umeshakuwa ni mlevi wa sukari (sugary addicted,
sugary craving) vyote hivi unaweza kujizuia kwa kukutana na mshauri wa afya
lishe atakupa maelekezo mazuri namna gani unaweza kukata sugar craving kiurahis
kabisa. Kumbuka kiwango kimoja cha kichecheo kikivurugika vyote vinavurugika
hivyo tunatakiwa kulinda sana kiwango cha insulin kuwa katika kiwango kizuri
muda wote ili kufurahia ndoa zetu.
2.
Kuepuka kabisa ulaji wa vyakula vya mafuta
Watu wengi sana huwa na fikra potofu kuwa chakula chochote cha mafuta ni
kibaya, na hivyo hujizuia sana kula vyakula hivyo kwa kuogopa kunenepa, napenda
nikwambie kuwa hakuna adui mkubwa wa magonjwa yote kama SUKARI hivyo vyakula
vya sukari ndio chanzo cha magonjwa mengi ya tabia ambayo ni magonjwa sug hapa
duniani, ndio chanzo cha uzito mkubwa kupita kiasi,kitambi,shinikizo la
damu,kisukai,upungufu wa nguvu za kiume,uvimbe kwenye kizazi,mzunguko mbaya wa
hedhi,ugumba,utasa nk hivyo basi kuna usemi unasema “SIO MAFUTA YANAKUFANYA
MGONJWA, BALI SUKARI NDIO INAKUFANYA ULEMEWE NA MAGONJWA”
Tafiti zinaonesha kuwa ulaji wa vyakula yenye mafuta kidogo sana tafiti
zinaonesha kuwa vichocheo vya progesterone hupungua na kupelekea kupoteza nguvu
za kiume na matamanio kwa jinsia tofauti.
3.
Nyama na vyakula vyote vya kusindika viwandani
Napenda kusema kuwa ulaji wa vyakula hivi sio ufahali katika familia
yako, bali ni uzembe katika uandaaji chakula katika familia yako, kuna usemi
unasema kuwa, ukitaka uishi kwa bajeti kubwa katika familia yako, kula vyakula
asili ambavyo babu zetu walikula enzi zile (EAT ORGANIC) ndio maana watu wengi
hawapendi kula vyakula asili, wanatafuta vyakula vilivyo sindikwa kwani havina
gharama kubwa. Kuna usemi unasema, unapokuwa upo jikoni unandaa chakula chako
kwa familia yako, unatakiwa ujiulize kwa nini vyakula hivi vya kusindika vina
bei rahisi kiasi hiki?
Ulaji wa vyakula hivi,siku zote huenda kuangamiza bakteria rafiki (Normal
flora) pia wengi hupendelea kuita gut probiotics na unapokuwa umewaangamiza
hawa ndio chanzo cha magonjwa yote kwani katika Makala zangu zilizopita nilieza
namna gani mfumo wa chakula unaweza kuwa chanzo cha afya bora yako, na chanzo
cha magonjwa yote mwilini mwako. Unapokuwa umeangamiza hawa viumbe katika mfumo
wa chakula kwa sababu ya vyakula ambavyo wao, hawavitambui, unakuwa ni mtu
wakushambuliwa na maradhi nyemelezi yote na kudhoofisha ukuta wa mfumo wa
chakula na hatimaye unaweza kuanza kupenyeza sumu (toxins), bakteria wabaya
kama E. Coli, vyakula ambavyo havijameng’enywa vizuri na protini zingine kama
gluten ambazo ni hatari kwa afya yako. Hivyo kama wewe umekuwa ukisumbuka na
nguvu za kiume na umekuwa ni mlaji mzuri sana wa vyakula hivyo, hakikisha una
viepuka kuwa mtu unayependa vyakula asili, vitarudisha uhalisia wa mfumo wako
wako wa chakula kwa kuondoa tatizo la tumbo kujaa gesi na choo kuwa ngumu.
4.
Sumu mbali mbali kutoka kwenye mazingira
Watu wengi sana wanapokuwa wanazungumzia tatizo la nguvu za kiume
wanasahau kuahusisha mahusiano yaliyopo kati ya upungufu wa nguvu za kiume na
mazingira yako. Najua kuwa tumekuwa tukijishughurisha na shughuli mbali mbali
ambazo zinatufanya tugusane na sumu mbali mbali, mfano madini ya mercury ambayo
sasa yapo kila kona katika biashara zetu, madini ya lead haya ni madini mazito
na hatari sana kwenye kudhoofisha utendaji kazi wa mwili wako, kukuletea msongo
wa muda mefu na mengine mengi ambayo yanapelekea kupoteza nguvu za kiume. Kwa dunia
ya sasa ya viwanda huwezi kuziepuka sumu kama hizi mwilini mwako, ni jukumu
lako kuhakikisha unajijengea mazoea ya kuondoa sum nzito hizi na mionzi mbali
mbali katika mwili wako na hatimaye kuimarisha afya yako.
Najua umejifunza kwa nini sasa una upungufu wa nguvu za kiume au huna
kabisa nguvu za kiume basi ningependa ijifunze jinsi gani unaweza kuhakikisha
unaondokana na tatizo hili na ukafurahia ndoa yako na mahusiano yako kuanzia
sasa, naomba basi nikuokoe katika tatizo hilo kwa kusoma njia tano za kurudisha
nguvu za kiume
NJIA SABA ZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME
Najua umekuwa ukisumbuka kila siku kufurahia ndoa yako, hadi imefikia
hatua mbaya, najua umekuwa mnyonge na mwoga wa kugundulika kwa mwenza wako kuwa
unasumbuka na tatizo hilo, umejaa woga, umegubikwa na msongo wa mawazo na
umekuwa ukizunguka kila sehemu upate msaada na hatimaye umekuwa ukitoa pesa
bila hata kurudisha furaha ya ndoa yako na nafsi yako! Pole lakini elimu ni
bora kuliko yote yaliyokupata ndugu, hebu soma hiki ambacho nimekuwa nikipewa
asante kila siku na wagonjwa wangu wewe pia uwe miongoni mwao.
1.
Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi,vya
kusindika, vyenye vionjo vya sukari,rangi na radha katika afya yako kwani
vyakula hivyo ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha
nguvu za kiume. Kula vyakula asili, nafaka ambayo haijakobolewa,matunda kwa
wingi ambayo hayasagwa yenye nyuzi nyuzi nyingi na pia juice ya matunda na
mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utafurahia ndoa
yako. Anza kuanzia leo rafiki
2.
Epuka pombe katika maisha yako yote kwani tafiti
zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini
inakunyima uwezo wa kufanya tendo la ndoa! Najua utashangaa lakini ndivyo
ilivyo, kuna usemi wa kiingeleza unasema, “It provokes the desire, but it takes away
the performance,” sio hayo tu
mpendwa pombe pia sugu, ni chanzo cha msongo wa mawazo na kukupelekea kukosa kabisa hamu ya tendo la
ndoa
3.
Fanya mazoezi ya kutosha. Watu wengi wamelemewa
na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda sehemu mbali
mbali kama vile ubongo,ini,figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako
ufanye kazi katika uhalisia wake. Hivyo basi magonjwa mengi ya msunguko wa damu
ni pamoja na nguvu za kiume kwani kama hufanyi mazoezi mwili wako unadhofika na
kukosa uwezo wa kuhimili ndoa yako pia inapunguza nguvu za kiume. Basi
ningependa kuwa kwa wale wazee siku hizi kuna vituo mbalimbali ambavyo
vitakusaidia mwili wako kuwa imara na kurudisha uwezo wako katika tendo la ndoa
kupitia mazoezi. Unaweza pia kuwasiliana nami nitakupa taratibu za kufuata
kukusaidia uanze mazoezi ya viungo kwa kutumia mashine maalumu kwa umri wako
ambazo zitasaidia kuimarisha mwili wako. Mazoezi huimarisha mwili wako na
kuweka mbali mwili wako na maradhi mbalimbali yanayo sababishwa na uzembe
katika mazoezi, usisumbuke kufanya mazoezi yenye kuumiza mwili wako, wasiliana name
kwanza kabla ya kufanya lolote.
4.
Rudisha Virutubisho ambavyo vimepotea mwilini
mwako
Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki,chuma, selenium, manganese
na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi
katika kiwango stahiki kwani huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes
kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako.
Unaweza kupata madini haya yote kutoka kwenye mboga za majani kama wewe
ni mvivu basi unaweza kunywa juice inayotokana na mboga mboga kama
kabeji,spinachi kale, nk. Kwa wale ambao ni kaz sana kuhimili zoezi hilo
unaweza kujipatia kirutubisho hicho ofsini kwetu ambacho kina madini yote hayo.
5.
Ondoa mafuta mabaya amabyo yanapunguza utendaji
kazi wa mzunguko wa damu, unaweza kuondoa kolestero mbaya mwilini mwako kwa
kutumia mafuta ya omega 3 ambayo unaweza kula vyakula vyenye mafuta haya kama
samaki kwa wingi, flaxseeds, blackseeds ni baadhi ya vyakula ambavyo vimekuwa
vikionekana kwenye nukuu za habari kuwa ni vyakula vyenye uwezo mkubwa wa
kusafisha mafuta mabaya mwilini mwako.
Unaweza pia kufika ofsini kwetu kama utahitaji mafuta haya yaliyotengenezwa
kitalamu utayapata na yatakusaidia.
6.
Ondoa Sumu kwa kutumia viondoa sumu. Kuna sumu
aina kuu tatu ambazo mimi huwa napenda kuziongelea siku zote na kushughurika
nazo kwa wagonjwa wangu kama zifuatazo,
-Sumu ambayo inatokana na
mabaki ya hewa ya oksijeni yani Free radicals ambayo ni moja wapo inaweza
kuumiza seli za mwili wako na kusababisha seli zako kubadili mtazamo wa ukuaji
na kuendelea kuzalishwa seli mbovu na hatimaye zinaweza kupelekea hata kupata
kansa.
-Sumu ambazo tunazipata
kutoka katika mazingira yetu ya kazi kwa kukutana na metali nzito kama lead, na
mercury ambazo ni kizuizi kikubwa sana katika utendaji wa mwili wako, pia sumu
inayotokana na mionzi mbalimbali inayotokana na kuchokozwa kwa miamba ya ardhi
( Earth’s crust)
-Sumu inayotokana na vyakula
tunavyokula ambavyo huenda na kuathiri mfumo wako wa chakula na hatimaye
kuharibu ulizi wa mwili wako katika mfumo wa chakula. Afya yako huanzia katika
mfumo wa chakula na magonjwa yote huanzia katika mfumo wa chakula.
Basi unaweza kuondoa sumu hizo kutokana na visababishi vyake kama nilivyo
eleza. Unaweza ukajipatia huduma hii kwa kutumia njia kuu zifuatazo
-Tunakupatia package ya siku 30 ambayo napenda kuitambulisha kwako pia
utumie kama utaona itakufaa kama wengine SEX DRIVE ENHANCING PACKAGE ambayo
itakuondolea sumu zote za free radicals na metali nzito za aina zote na
kurudisha utendaji kazi wa mwili wako na kurudisha nguvu za kiume.
-
Kwa wale ambao umri kidogo umeenda hawawezi kufanya mazoezi vizuri ningependa
ufike ofsini kwetu tuje tukusaidie tatizo lako mpendwa.
Najua umejifunza mengi sana kuhusu tatizo la nguvu za kiume,
sasa napenda nitimishe kwa kukuambia kuwa suluhisho la nguvu za kiume lipo
kabisa ni kuhakikisha tu, unaliondoa tatizo hilo kwa kufuata elimu hii, na kama
unaona elimu hii ni muhimu kwako basi unaweza pia kutupigia na kufika kwetu
moja kwa moja kupata suluhisho la tatizo lako
Unaweza tembelea
Whatsapp: 0767074124
Email:boazkitundu@gmail.com
DAR ES SALAAM
0 comments :
Post a Comment