-->

MESSI APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA(GLOBE SOCCER AWARDS IN DUBAI WINNERS 2015)


Lionel Messi akipokea tuzo yake ya heshima ya mchezaji bora wa mwaka kutoka Globe Soccer, Dubai

  • Lionel Messi ametangwazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwenye tuzo za Globe Soccer
  • Barcelona imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka
  • Tuzo ya Player career imekwenda kwa Andrea Pirlo na Frank Lampard
  • Jorge Mendes amepewa tuzo ya wakala bora wa mwaka
Super Star wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya heshima iliyotolewa na Globe Soccer, Dubai.
Legend wa Italia Andrea Pirlo akipokea tuzo yake ya heshima baada ya Globe Soccer kutambua mchango wake kwenye soka
Mabingwa wa La Liga Barcelona ambao walitwaa mataji matatu (treble) msimu uliopita walitangazwa kama klabu bora ya mwaka wakati Josep Maria Bartomeu (Rais wa klabu ya Barcelona) alitangazwa kama rais bora wa klabu wa mwaka.
Mchezaji anayekipiga pamoja na Pirlo, Frank Lampard wanaokipiga kwenye timu ya New York City akipokea tuzo kama ya Andrea Pirlo
Mshambuliaji huyo wa Argentina, alifanikiwa kupachika mabao 58 na kuisaidia Barcelona kunyanyua ndoo tatu msimu uliopita.
Jorge Mendez ambaye pia ni wakala wa star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akipokea tuzo ya wakala bora wa mwaka
Wakongwe wanaokipiga kwenye klabu ya New York City Andrea Pirlo na Frank Lampard wao walitwaa tuzo ya heshima kutokana na mchango wao katika soka (Player Career Award).
Kocha wa Ubelgiji Marc Wilmots (kushoto) akipokea tuzo ya kocha bora wa mwaka
Jorge Mendes ambaye pia ni wakala wa super star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yeye alitwaa tuzo ya wakala bora wa mwaka, kocha wa Ubelgiji yeye akatangazwa kama kocha bora wa mwaka.
Tuzo 2
Wakati huohuo klabu ya Benfica ilitwaa tuzo ya Best Academy of the Year, Ravshan Irmatov alitajwa kama mwamuzi bora wa mwaka .
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment