Serikali imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.
Makontena hayo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61, DICD 491, JEFAG 1, 450, AZAM 295, PMM 779, AMI 4384, TRH 4,424 ambazo kodi yake ni zaidi ya sh.bilioni 47.
Magari 2019 yalitolewa bila kulipa kodi katika kampuni za TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SILVER 97, MASS 171, HESU 1359 na kunyima nchi kodi yenye thamani zaidi ya Tsh.bilioni moja (1).
Waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kukamatwa leo ni John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally ,Masoud Seleman na Benadeta Sangawe.
Wanaotafutwa kwa tuhuma za kusababisha upotevu wa kodi za serikali katika bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.
0 comments :
Post a Comment