Dr. Boaz Mkumbo MD
Ni dhahiri kuwa wagonjwa wengi siku hizi wamekuwa wakikumbwa
na tatizo hili la kupooza ambalo wengi huwakumba ghafla wakiwa hawana ufahamu
wowote nini ambacho kimetokea.
Kabla zijakuelimisha mengi mpendwa msomaji wangu wa Makala zangu,
basi leo nakupa maana ya baadhi ya maneno haya:
1.
KUPOOZA
Hii ni ile hali ya kiungo kupoteza utendaji
kazi wake kwa sababu ya neva za fahamu kuathiriwa.
2.
KIHARUSI AU STROKE
Hii ni ile hali ya ubongo kupata hitilafu
katika kupokea damu na hatimaye kupelekea kupooza kwa viungo baadhi au mwili
mzima. Na endapo seli za ubongo zikikosa damu na oksijeni kwa dakika 3 zinaanza
kufa na kupoteza utendaji kazi wake na endapo hili tatizo lispo shughurikiwa
ndani ya masaa matatu dalili zake zinakuwa zimefikia pabaya sana katika
matibabu.
Sasa basi ningependa kuongelea kidogo
kuhusu ugonjwa huu na jinsi gani unaweza kujizuia.
SABABU ZISIZO EPUKIKA
Napenda kusema kwamba, Katika kitabu cha
The China Study kilicho andikwa na Prof. Collin Campbell kinasema kwamba, kila
binadamu ana chembe chembe za vina saba yani DNA za urithi kutoka kwa wazazi
wetu ambazo zinarithishwa kila kizazi. Hivyo kila mtu ana viini vya urithi vya
magonjwa mbalimbali kutoka kwa wazazi wetu, ni jukumu lako kufanya chembe
chembe hizo zijioneshe wazi wazi. Hivyo bwana Campbell ambaye ni mtafiti
mashuhuri wa lishe na magonjwa alisema kuwa, ni jukumu lako wewe kuuchokoza
mwili wako uwezo kuonesha magonjwa ambayo umeyarithi kutoka katika ukoo wenu.
Endapo ukiishi maisha ya kiafya, kula vizuri vyakula vya asili hutasumbuka na
magonjwa tabia kama kisukari,shinikizo la damu,uvimbe kwenye kizazi,ugumba,kansa
nk.
Kwa sababu tumeshindwa kuishi maisha ya
uhalisia wetu,tunaishi kwa kufurahia vyakula vilivyofanyiwa marekebisho na
binadamu na kufurahia bei yake ilivyo ndogo katika kiwango cha kujitosheleza,
Basi swali la kujiuliza ni kwa nini vyakula hivyo vya viwandani vinauzwa bei ya
chini sana kuzidi vyakula asili? Hebu nenda leo ukanunue nyanya ambazo unaweza
kukamua ukapata chupa moja ya 400mls! UTAGHARIMIKA PESA KUBWA KULIKO YULE ALIYENUNUA
Nyanya iliyotengenezwa kiwandani na kuwekwa kwenye chupa maalumu, Jiulize tena
Kwa nini vinauzwa bei ya kiwango cha chini kiasi hicho?
Mwenendo huo wa maisha ya ulaji vyakula vya
viwandani,vinywaji vyenye sukari nyingi,radha,rang ink, unatufanya tuwe na
vihatarishi vya kupata ugonjwa wa kupoooza bila kuwa na uwezo wa kuepuka hadi
pale tutakapo badili mwenendo wa maisha yetu.
1.
UMRI
Tafiti zinaonesha kuwa kadri umri wako unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo
unavyozidi kuwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la kupooza. Umri Zaidi ya
miaka 50 upo katika hatari kubwa sana ya kupata magonjwa yatakayokupelekea
kupata kiharusi. Kwani kiharusi ni ugonjwa moja wapo utakao kupelekea kupooza
kwa baadhi ya viungo vya mwili wako na haimaye mwili mzima.
Hivyo kama wewe bado hujafikia katika umri huu, basi ni wakati wa kuishi
katika lishe asili Inatoka katika
mashamba yetu ya wakulima.
2.
JINSIA
Tafito zinaonesha kwamba wanaume wako hatarini sana kupata kiharusi
ukilinganisha na jinsia ya kike. Lakini pia tafiti zinaonesha kuwa kati ya
mwanamke na mwanaume, mwanamke ndiye yupo hatarini sana kupata kifo kitokanacho
na kiharusi. Hivyo endapo mwanamke akipatwa na kiharusi maendeleo yake kuanzia
anapopatwa na tatizo huwa sio mazuri sana ukilinganisha na mwanaume. Hivyo mwanamke
huwahi kukutwa na kifo Zaidi ukilinganisha na mwanaume anaweza kukaa muda mrefu
sana.
3.
URITHI
Kuna watu wenye historia kuwa katika ukoo wao kuna watu wenye matatizo ya
kiharusi au babu, bibi alikumbwa na tatizo hilo. Hivyo hata wewe unaweza ukawa
hatarini kupata tatizo kama hilo endapo tu maisha unayo ishi nayo yakiwa ni
maisha yasiyo jumuisha lishe ya asili ninayopenda kuita lishe ya dawa.
4.
KAMA UMESHAWAHI KUPATWA KIHARUSI KIDOGO
Hii ni aina ya kiharusi inayotokea kwa muda mfupi na kupotea. Muda mwingine
huwa ni vigumu kutofautisha na kiharusi chenyewe. Maana kiharusi kidogo
(Transient Ischemic Attach) husababisha pia viungo kupoteza utendaji kazi wake
na inaweza pia kuathiri utendaji kazi wa ubongo kiakiri pia. Hivyo kama
umeshaga wahi patwa na TIA kipindi cha nyuma, uwezekano wa kupata tena ni
mkubwa sana, na unaweza kupata kiharusi kabisa chenyewe.
Hapo juu nimesema kuwa ni vihatarishi visivyozuilika LAKINI ni kwa wale
wasioweza kubadili mienendo ya maisha ya kifahari na kujiepusha na magonjwa
tabia kama kisukari,shinikizo la damu na kiwango kikubwa cha lehemu mwilini
mwako
SABABU UNAZOWEZO KUZISABABISHA WEWE MWENYEWE NA KUKUPELEKEA KUPATA
KIHARUSI ( STROKE)
1.
MAGONJWA YA MOYO
Magonjwa ya moyo kwa umri Zaidi ya miaka 60 imekuwa ni kawaida kutokana
na miili yetu kuwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini mwetu na miili yetu
kuwepo katika mazingira ya kupokea vyakula visivyo vya msingi katika kuboresha
utendaji kazi wa mwili wako na tofauti na kuharibu uwezo wa mwili wako kufanya
kazi ipasavyo.
Moja wapo ya
magonjwa yanayopelekea kupata kiharusi, ni pale moyo wako unaposhindwa
kutengeneza umeme wa kutosha kutoka juu kwenye vyumba vya moyo viitwavyo Atria
na hatimaye kusambaa kwenye vyumba vya chini vya moyo viitwavyo Ventriko. Hivyo
basi napenda kukuambia kuwa, moyo hutengeneza umeme, na umeme huo huzunguka
kwenye sakiti ya umeme wa moyo, sakiti hio huanzia kwenye vyumba vya juu vya
moyo na kushuka vyumba vya chini na hatimaye kusambaa katika misuli yote ya moyo
na hatimaye kusukuma damu kutoka kwenye moyo. Hivyo kunapokuwa kuna hitirafu
katika utengenezwaji wa umeme kuanzia sehemu husika, umeme unatengenezwa
usiotosheleza na unatoka sehemu mbalimbali (sio maalumu) unajikuta misuli ya
moyo inapata umeme kutoka katika vyanzo tofauti na umeme huo hautoshelezi
kuweza kusukuma damu ipasavyo. Ugonjwa huu kwa lugha ya kiratini tunaita Atrial
Fibrillation. Hivyo moyo wako unapokuwa na tatizo hili, hata mapigo ya moyo
hubadirika. Njia pekee ambayo unaweza ukajigundua kuwa una tatizo hili, ni
kuangalia kiashiria cha mapigo ya moyo sehemu mbali mbali kama shingoni,juu ya
mkoni wako karibu na kiganja kama mapigo ya moyo yanaenda sawa au laa! Pia
unaweza kwenda Zaidi kufanya uchunguzi kama kipimo cha ELECTROCARDIOGRAM (ECG) unaweza
kupata majibu halisi kuwa umeme huo unajitosheleza au laa! Na unatengenezwa
kutoka katika chanzo kimoja au laa! Pia moja ya sababu moja wapo ni kuangalia
misuli ya moyo na kiwango cha damu kinachosukumwa na myo wako, ni vyema pia
ukipata kipimo kingine cha moyo kinaitwa ECHOCARDIOGRAM(ECHO) hiki kinakupa
taarifa zote za kiwango cha damu kinachosukumwa,ukubwa wa misuli ya moyo, na
taarifa zinginezo. Kumbuka vipimo hivi vinapatikana katika hospitali kubwa za
rufaa na vinategemea umahili wa mpimaji na msomaji wa majibu yako.
Ugonjwa huu wa moyo unaweza kusababisha kiharusi kwa sababu moja kuu
kwamba, pale moyo unaposhindwa kutenegeneza umeme wa kutosha kusukuma damu,
kutakuwa na mrundikano wa tamu kwenye moyo na damu hio inaweza kuganda na
hatimaye kusukumwa kwenda kwenye mishipa midogo ya ubongo na kusababisha
kizuizi cha damu kufika kwenye ubongo kwa sababu ya kutwama kwa damu iliyo
ganda. Hivyo ndivyo unaweza kupata kiharusi endapo moyo wako hautengenezi
vizuri umeme wake.
2.
KIWANGO KINGI CHA CHOLESTERO(LEHEMU) MBAYA
MWILINI MWAKO
Lehemu kwa tafsiri nyepesi ni fati(mafuta) ambayo ipo kama nta ( wax) huzunguka
sehmu mbalimbali katika mwili wako kwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu.
Ikumbukwe Lehemu ina kazi kubwa sana miilini mwetu kama kutengeneza seli
za mwili na kutengeneza homoni za miili yetu na kazi zingine nyingi. Hivyo basi
ningependa kukuambia kuwa kuna ina kuu tatu za lehemu ambazo ningependa
kuzitaja kwa ufupi katika makundi makuu mawili, Lehemu mbaya ambayo inajulikana
kama Low density Lipoprotein (LDL) pia
na Triglycerides na aina ya pili ni lehemu nzuri ijuilikanayo kama Hingh density
Lipoprotein –HDL.
Lehemu inaweza kusababisha kiharusi kwa sababu ya tabia yake mbaya ya
kunasa kiurahisi kwenye kuta za mishipa ya ateri na hatimaye kupunguza kipenyo
cha mshipa wa damu au kuziba kabisa na hatimaye kuzuia damu kufika vizuri
katika ubongo na hatimaye ubongo hukosa damu na oxygen.
Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa nyama za aina yoyote ile, zina kiwango
kingi sana cha lehemu mbaya ambayo inaenda kutuathiri sana. Lakini pia tafiti
zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya mboga za majani, matunda vinasaidia sana
kuepukana na lehemu mbaya na kumaliza kabisa matatizo yanayo sababishwa na
lehemu mbaya mwilini mwako.
Rehemu hujulikana kama kisababishi kikubwa cha aina moja wapo ya kiharusi
kinachosababishwa na mishipa midogo ya damu kutopitisha damu na kuulisha ubongo
wako vizuri na hatimaye seli za ubongo huanza kufa nah ii hutokea baada tu ya
ubongo kukosa damu kwa muda wa dakika tatu.
Aina hii ya kiharusi huitwa ISCHEMIC STROKE (Ischemia, Ni ile hali cha
seli za mwili kufa Kwa kukosa oxygen, na Stroke ni kupooza). Hivyo Ischemic
stroke ni kupooza kunako sababishwa na kukosa hewa ya oksijeni kwenye ubongo
kwa sababu ya kukosa damu kwenye ubongo kunakosababishwa na kuziba kwa mishipa
midogo midogo inayopeleka damu kwenye ubongo.
Unaweza kuchunguza kiwango chako cha lehemu kama kingi au laa! Unaweza
kwa kuchunguza kitalamu kwa kuchukua sampuli ya damu na kupeleka maabala
(Biochemistry Lab) na hatimaye utapata majibu yako. Pia unaweza ukatumia vipimo
vingine vya picha vinavyopima kiwango cha lehemu mbaya moja kwa moja kwenye
mishipa ya damu Angiogram na pia unaweza kupima kwa kutumia Kipimo cha
kuangalia uzalishaji wa umeme kwenye moyo kwani lehemu ni chanzo kikubwa sana
cha kuharibu utendaji kazi wa moyo hivyo kipimo cha Electrocardiogram kinaweza
pia kutumika na kuangalia moja kwa moja.
Note: Napenda kutoa angalizo kuwa vipimo vingi ninavyotaja hapo ni
vikubwa sana na gharama yake kidogo kubwa na vingi vinapatikana hospitali ya
rufaa na kwenye vituo mbali mbali binafsi. Na hivyo wengi wenu mmekuwa
mkiniuliza kama Dr Boaz Mkumbo naweza kuwasaidia kwa hilo. Napenda kuwasaidia
kama ninavyokupatia elimu hii ya afya bure kabisa, ushauri wangu ni kwamba
vipimo vyote vya kitaalamu vinategemea na mpimaji na msomaji ana taaluma gani
katika kusoma majibu. Kama mpimaji akipotosha na daktari anayetibu atapotoka na
hapa ndipo madhaifu makubwa ya vipimo hivi vingi na ndio maana magonjwa mengi
tunashindwa kuyabaini mapema kwa kukosekana kwa ufanisi kwa watu wanaopima.
Sasa ningependa kukupa siri moja ya vipimo vyote nilivyo vitaja hapo juu, Vina
hitaji umahili mkubwa wa kusoma majibu, na vituo vingi binafsi havina watu
mahili wa kusoma vipimo hivi ,viko pale kama kitega uchumi kukushusha roho kuwa
umepima. Tatizo sio kupima, Kiu ni kugundua ugonjwa sahihi na utibiwe upone.
Ningependa kukushauiri kama unahitaji vipimo hivi, fika hospitali yenye
wataalamu wa kutosha wenye uwezo mkubwa wa kukupa majibu ya uhakika ya kukata
kiu yako.
- American Diabetes Association Inashauri kiwango cha LDL cholesterol kuwa
chini ya 100 mg/dl kwa watu wenye kisukari na chini ya 70 mg/dl kwa watu wenye
magonjwa ya moyo.
-Pia inashauri kuwa kiwango cha lehemu nzuri yani HDL iwe 50 mg/dl au Zaidi
kwa wanawake na kwa wanaume HDL iwe 40 mg/dl au Zaidi.
3.
SHINIKIZOLA JUU LA DAMU( HIGH BLOOD PRESSURE)
Shinikizo la damu ni msukumo wa damu ndani ya mishipa ya damu thidi ya
ukuta wa mishipa. Shinikizo la damu lenye takwimu ya Zaidi 140/90 mmhg kwa muda
mrefu utakuwa unastahili kuitwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu.
Shinikizo kubwa la damu husababisha kiharusi kwa kusababisha mishipa
midogo ya damu ya ubongo kupasuka na hatimaye damu kuvia kwenye ubongo. Aina hii
ya kiharusi huitwa Hemorrhegic Stroke. Aina hii ya kiharusi ni mara chache sana
kutokea na huwa ni nadra sana kukuta mtu ana aina hii ya kiharusi lakini ndio
aina nambari moja inayoweza kusababisha kifo haraka sana kwa mgonjwa. Kwani wagonjwa
wengi wanaopata aina hii ya kiharusi huwa maendeleo yao sio mazuri na wengi
hufika hospitali wakiwa hawajitambui kabisa.
Ugonjwa
wa Shinikizo la damu unazuilika kabisa kwa kufuata masharti machache kama haya
hapa chini:
- Ulaji wa vyakula vya madini ya potasiamu hadi kufikia 3900mg kwa siku kutoka kwenye ndizi,machungwa,matunda yaliyo kaushwa,viazi vitamu nk
- Ulaji wa Madini ya Calcium angalau 1200mg kila siku kutoka kwenye vyakula kama mtindi na maziwa ya kuwaida
- Ulaji wa vyakula vyenye magnesium angalau 420mg kwa siku kwa wanaume na 320mg kwa wanawake kutoka kwenye vyakula kama Spinachi, nafaka isiyokobolewa, Ndizi nk
4.
KUTOFANYA MAZOEZI YA VIUNGO
Mazoezi siku hizi yamekuwa yakitumiwa na watu pekee wanao hitaji
kupunguza mwili na kupunguza nyama uzembe ( belly fats) ,inapendeza sana wadada
wengi kuchukia kubadirika kwa miili yao unaotokana na ulaji wa vyakula visivyo
asili, Napenda kukuambia kuwa Mazoezi pekee sio SULUHISHO LA KUPUNGUZA MWILI
WAKO, NA WALA SIO SULUHISHO LA KUONDOA NYAMA UZEMBE. Bali siku ukijifunza
kubadili mwonekano wa sahani yako mezani utafurahia jinsi uzito unavyopungua! Najua
huamini, lakini unapokuwa unaanza safari ya kupunguza uzito na nyama uzembe
ujue ni safari nzito kama vile safari ya kutafuta pesa. Kupungua uzito sio
kurahisi ingekuwa rahisi wengi hawapendi wangekuwa wameshapungua ! Njia pekee
ni kujidhatiti na kudhubutu pekee katika kubadili lishe yako, mchawi mkubwa ni
sahani yako unayoiweka mbele yako kila utakapo kuweka kitu kinywani mwako.
Mazoezi huimarisha viungo na mzunguko wa damu na kusaidia mwili wako
kutoa taka ambazo zimepatikana kutokana na shughuli za mwili.
Tafiti zinaonesha kwamba watu ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha katika
umri mkubwa huwa hatarini kupata kiharusi aina ya Ishemic stroke
inayosababishwa na damu kutosukumwa ipasavyo katika mishipa ya damu na
kusababisha emboli kunasa kwenye mishipa
ya damu na kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo.
MAKUNDI MENGINEYO AMBAYO SITAPENDA KUYAELEZA KWA KINA LEO
5.
Walevi wa pombe na sigara
6.
Wanaotumia njia za uzazi wa mpango kwa muda
mrefu
7.
Watu wenye kisukari kwani kisukari na shinikizo
la damu ni bwana harusi na bibi harusi mara nyingi hutembea kwa umoja.
90 DAYS CARDIO FUNCTION-REVERSE PACKAGE
Hii ni program maalumu kwa wasomaji wetu ambao wamekuwa wakisumbuka na
magonjwa sugu kama kisukari,shinikizo la juu la damu n ahata shinikizo la chini
la damu, kiharusi n ahata tatizo la kupungua kwa utendaji kazi wa ubongo.
Hii
program imeandaliwa na Boaz Mkumbo ambapo inawafaa wale wachache wanaohitaji
msaada wangu pale walipofikia kutumia elimu hii ya afya ambayo nimekuwa
nikiitoa kila siku.
NDANI YA CARDIO FUNCTION
REVERSE PACKAGE
1.
Unajipatia msaada wa kupata Suluhisho la kuondoa
lehemu zote mbaya mwilini mwako na kuimarisha mzunguko wa damu kwenda sehemu
mbalimbali za mwili na kuimarisha damu inayoenda kulisha ubongo.
2.
Utajipatia Kiondoa sumu makini kabisa chenye
kuzuia mchakato unaendelea mwilini mwako ( Gut and systemic Inflammation)
chenye kusheheni madini mengi ambayo ni catalyst ya shughuri nyingi za mwili
madini haya husaidia kuupooza mwili kutoka katika mpambano wa maradhi mbali
mbali yanayoendelea mwlini mwako, Madini mengi ya Manganeze,zinc,selenium,Iron
na mengine mengi kwani kimekuwa ni chakula nambari tatu kama lishe bora duniani
3.
Unaweza kupatiwa ushauri kwa wale waliotayari
pata tatizo la kupooza kutokana na kiharusi na presha yako haijakaa sawa,
Utapewa huduma nzuri namna gani unaweza pia ukanufaika na mazoezi ya viungo na
bidhaa zetu unapokuwa katika matibabu chini ya ushauri wetu.
4.
Napenda kuwaambia kuwa msaada huu ndani ya
package hii ya siku 90 tutakusaidia endapo tu , unahitaji kwani wengi
wanafurahia huduma zetu za tiba asili na pia ushauri tunatoa kwa watu wenye
matatizo ya magonjwa haya sugu.
Napenda kukushukuru kwa kusoma elimu hii ya afya, najua
umejifunza kitu, mungu akubariki usisahau kulike ukurasa wangu facebook Dr Boaz
Mkumbo MD.
Email: boazkitundu@gmail.com
Whatsapp: 0767074124
0 comments :
Post a Comment